×

Mtambo wa Mabao Gerd Muller Afariki Dunia

MUDA mfupi uliopita leo Agosti 15 , Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imetangaza kifo cha mkongwe wao wa soka, Gerd Muller ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75.

 

Katika posti yao ya hisia kali kupitia ukurasa wao wa Twitter, Bayern Munich wameandika; “Leo ulimwengu wa FC Bayern umetikisika mashabiki wanamuomboleza bingwa wa soka wa Ujerumani mwenye rekodi nyingi za muda wote Gerd Muller, ambaye amefariki mapema leo Jumapili akiwa na umri wa miaka 75.”

 

Muller alizaliwa Novemba 3, 1945 mjini Nordlingen alikuwa mchezaji muhimu na mfungaji bora wa zamani wa Ujerumani ufungaji bora wa Muller ulijidhihirisha wenyewe.

Alifunga mabao 68 katika mechi 62 akiwa na Timu ya Taifa alifunga mabao 365 katika michezo 427 katka Ligi ya Bundesliga na mabao 66 ya kimataifa katika michezo 74 kwa ngazi ya klabu za Ulaya.

 

Mwaka 1970, Muller alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwaka wa Ulaya baada ya mafanikio msimu huo akiwa na Bayern pia alifunga mabao 10 kwenye Kombe la Dunia 1970.

 

Alianza kucheza soka katika Klabu ya TSV 1861 Nordlingen, alijiunga na FC Bayern Munich mwaka 1964 ambapo aliungana na wachezaji wenzake mahiri kama Franz Beckerbauer na Sepp Maier.

 

Alishinda mataji mengi miaka ya 1960 na 1970  alishinda ubingwa wa Ujerumani mara 4, ubingwa wa Ulaya mara 3, ubingwa mabara mara 1 na ubingwa wa Mabingwa wa Ulaya mara 1.

 

Baada ya Bundesliga alikwenda Marekani ambapo alijiunga na Fort Lauderdale Strikers mwaka 1979 iliyoshiriki Ligi ya Marekani Kaskazini na akafunga mabao 38 katika nyakati zote anaichezea timu hiyo.

 

Baada ya kustaafu alijikuta mlevi wa kupindukia, hivyo marafiki zake walimpa ushauri na kurudi katika hali yake, alipata kazi ya ukocha Bayern Munich II ambapo alifanya kazi hadi hali yake kiafya ilipoanza kutetereka.

Ama kweli mtambo wa mabao umeondoka!

Stori : Sifael Paul

Leave a Comment