
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa na kwamba wanawasiliana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kueleza kwamba ni pigo kubwa kwao.