×

Taliban: Hatutalipiza Kisasi

MSEMAJI wa Kundi la Wanamgambo la Taliban, Zabiullah Mujahid amesema vyombo vyote vya habari nchini humo viendelee kurusha matangazo kama kawaida lakini ameonya kuwa visirushe jambo lolote lililo kinyume na Uislamu ama kinyume na matakwa ya Taifa hilo.

 

Aidha, Mujahid amesema hawatolipiza kisasi kwa mtu yeyote,wawe ni Wanajeshi, raia au wale wote waliofanya kazi na Majeshi ya kigeni. “Hatutokagua nyumba ya mtu yeyote. Mji wa Kabul hali yake itarejea kwenye kuwa kawaida hivi karibuni….”

Leave a Comment