×

Makambo Awatangazia Vita Simba

YANGA imefanya usajili wa wachezaji kadhaa hadi sasa kuelekea msimu ujao wa 2021/22, kati ya hao, wapo wazawa na wa kimataifa.

 

Kwenye orodha ya nyota wote waliotambulishwa mpaka sasa katika kikosi hicho, yupo Heritier Makambo ambaye amerudi baada ya awali kucheza msimu wa 2018/19.

 

Raia huyo wa DR Congo, msimu mmoja aliocheza Yanga, alifunga mabao 17 katika Ligi Kuu Bara na kuwa kinara wa mabao kwenye kikosi hicho.

 

Nyota wengine waliotambulishwa ni Djuma Shabani, Jesus Moloko, David Bryson, Dickson Ambundo, Erick Johora, Khalid Aucho, Djigui Diarra, Yusuph Athuman na Fiston Mayele.

Usajili wa Makambo, umewafanya mashabiki wengi wa Yanga kuwa na matumaini naye makubwa kwamba atawabeba msimu huu wa 2021/22 katika kushinda mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA waliyoyakosa kwa muda mrefu.Makambo akiwa ni mmoja wa wachezaji waliosafiri na kikosi hicho juzi Jumapili kwenda kambini Morocco, ametoa ahadi kubwa kwa mashabiki wa Yanga.

 

Akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar, muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Morocco, Makambo alifanya mahojiano na Spoti Xtra na kufunga mambo kadhaa.

Katika mahojiano hayo, Makambo aligusia ishu ya kubeba makombe, akiwatangazia vita wapinzani wao wakiwemo Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

 

UNA KIPI CHA KUWAAMBIA MASHABIKI WA YANGA?
“Namshukuru Mungu kwa
kupata nafasi nyingine ya kuwa ndani ya Yanga, nawaambia mashabiki wasubiri kuona makubwa kwani tutapambana sana

 

KUNA MABADILIKO YOYOTE YANGA YA SASA NA ILE ULIYOKUWEPO?
“Karibia kila kitu ndani ya Yanga
ni kipya, ninajitahidi kuzoea mazingira maana Yanga ni timu kubwa, binafsi najivunia kuwa hapa.

 

UNAONAJE USHINDANI WA NAMBA NDANI YA YANGA?
“Ushindani utakuwa mkubwa
sana msimu ujao, ukiangalia kila mchezaji ni mzuri, nitajitahidi sana kupambana kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza, na kupitia pre-season nahisi nitaweza kujiweka sawa kufanya vizuri.

 

TUTEGEMEE UTAFUNGA MABAO MANGAPI MSIMU UKIANZA?
“Siwezi kusema moja kwa
moja ni mangapi kwani ninaweza kusema 20 yakawa 25, lakini watu waelewe tu kwamba nitapambana kufunga mabao mengi.“Mimi ni straika na nina mipango ya kuwa mfungaji bora, hivyo nitapambana kuwa mmoja kati ya wafungaji bora, maana hayo ndio malengo yangu siku zote.

 

UMEJIPANGAJE KWA MICHUANO YA KIMATAIFA?
“Ndani ya Yanga hii ni mara
ya kwanza nashiriki michuano ya kimataifa, lakini nikiwa timu zingine nimewahi kushiriki.“Kutokana na uzoefu wangu, hakuna mashindano mepesi, lazima tutakutana na ugumu, lakini itategemea na maandalizi ya timu. Tutajiandaa vizuri.

 

TUTARAJIE YANGA ITAFIKA HATUA GANI KIMATAIFA?
“Yanga ni timu kubwa na
kutokana na pre-season hii ilivyo nzuri na usajili
uliofanywa, ninaimani tutafika

mbali sana.

VIPI KUHUSU KUBEBA MAKOMBE?
“Makombe yote
tutakayoshiriki, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA) lazima tuyachukue,” anasema Makambo.

STORI: CAREEN OSCAR

Leave a Comment