
WATU wawili wamefariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Sea kugongana na lori katika kijiji cha Unyenye Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imesababishwa na mwendokasi na uzembe wa dereva wa basi, ambapo alikuwa akifukuzana na madereva wenzake wa mabasi mengine mawili yaliyotoka pamoja katika Stendi ya Majimoto mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Benjamini Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema taarifa zaidi zitatolewa baadaye huku Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe, Martine Lohay akithibitisha kupokea majeruhi 25 na miili ya watu wawili waliofariki kutokana na ajali hiyo.