
Rais Samia Suluhu Hassan kesho Agosti 24, 2021 anatarajiwa kufungua kikao kazi cha siku tatu cha Maofisa Wakuu wa Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa jeshi la Polisi, SACP David Misime ameyasema hayo leo na kueleza kuwa kikao hicho kinatarajia kuanza kesho na kuongeza kuwa kufunguliwa kwa kikao kazi hicho na Rais Samia, kutatoa fursa kwa makamanda hao kufanya tathmini ya utendaji kazi, kuona mafanikio na changamoto na kutoka na mikakati mbalimbali ya kutekeleza jukumu lake kuu la kulinda maisha ya watu na mali zao.