×

Aliyekuwa Mmiliki wa Mabasi ya Mtei Afariki Dunia

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Manyara, James Mtei ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Jambo Express, ambaye pia awali alikuwa mmoja kati ya wakurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Mtei, amefariki dunia ghafla, jana Jumanne Agosti 24, 2021.

 

Ndugu wa marehemu aitwaye Elly Mtei amesema kaka yake amefariki ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa nyumbani kwake. Amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwake Mrara mjini Babati.

 

Leave a Comment