×

Mobetto Awaka na Uzi Mpya wa Simba

IKIWA ni dakika chache baada ya Klabu ya Simba kutangaza uzi wake mpya utakaotumika katika mashindano mbalimbali msimu ujao, Mrembo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto ametupia picha zake kadhaa akiwa ametinga uzi huo.

Jezi aliyovaa Mobetto ni ile ambayo imetengenezwa maalum kwa ajili ya wadada.

Tayari Simba imesema jezi zake mpya zinapatikana kwenye maduka ya Vunjabei yaliyopo Dar es Salaam na mikoani hivyo kuwaomba mashabiki wake wanunue jezi hizo.


Leave a Comment