×

Ndoa ya Ben Pol Mambo Yanoga

DAR: UKISIKIA mambo ni moto, basi ujue ni moto kwelikweli baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ na mchumba wake Anerlisa Muigai kuanza mikakati ya ndoa mapema kabla hata ya Corona kuisha.

 

Ben Pol ambaye Aprili mwaka jana alimchumbia mrembo huyo mwenye ‘mapene ya kutosha’ kutoka nchini Kenya, ameainisha ukweli kuwa tayari taratibu za awali zimeshakamilika na hivi karibuni watatangaza muda sahihi wa kufunga pingu za maisha.

 

Akipiga stori na IJUMAA Wikienda, Ben Pol alianza kwa kusema kuwa, kwanza amehamia Mbezi Beach baada ya kuhama alikokuwa amepanga awali.

 

Alisema kuhusu ndoa, Watanzania na mashabiki zake wasubiri, kwani muda mfupi ujao atatangaza lini na wapi ndoa hiyo itakapofungiwa.

 

“Kuhusu ndoa na mchumba wangu, siwezi kusema kuwa nimeshafunga au bado kwa sababu ni vitu vya kifamilia zaidi na pia sasa hivi nitakuwa naishi sana Kenya na kazi zangu za muziki wamezipokea sana, kwa hiyo nitafanyia kazi kule.

 

“Tanzania nitakuwa nakuja kwa sababu familia yangu ipo huku, wazazi wangu pamoja na ndugu zangu.

“Kwa hiyo, kuhusu ndoa vipo chini ya kapeti, bado sihitaji nivitoe hadharani. Ila niwaambie tu mashabiki zangu kuwa muda si mrefu tutawapa taarifa,” alisema.

 

Alisema kuhusu muziki, anatarajia kutoka tofauti na zamani kwa kuwa sasa anatarajia kutoka kijamii zaidi.

“Nitazungumzia sana hili janga la Corona ambalo limeikumba dunia pamoja na changamoto nyingine zinazoihusu jamii,” alisema Ben Poul.

 

Ben Poul alianza mahusiano na Anerlisa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kiwanda cha maji huku Mama yake aitwaye Tabitha Kiranja ambaye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha bia nchini humo, naye ni bilionea namba 4 kwa wanawake nchini Kenya.

Stori: INEEMA ADRIAN , IJUMAA Wikienda

Leave a Comment