×

Chaz Baba: Mwanangu atafuata nyayo zangu!

CHAZBABA4Hakuna kinachoshindikana hapa zaidi ya kuendelea kusonga mbele na safu yetu hii ya Mpaka Home Next Level, tukiwa na lengo mahususi kabisa kwa ajili ya kukuburudisha kila kukicha.

Wiki hii safu hii imemtembelea Staa wa Muziki wa Dansi Bongo, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, nyumbani kwake Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kubahatika kumpiga picha mbalimbali akiwa na mkewe Rehema Sospeter Marwa na mwanaye mdogo Carson.

Chaz Baba amemtabiria mwanaye huyo kuja kuwa mrithi wa kazi yake ya uimbaji kwani amekuwa akimfuatilia nyendo zake na amegundua wazi kuwa siku moja atakuja kuwa mwanamuziki bora hapa nchini..

Chaz Baba kwa sasa bado anaitumikia Mashujaa Band yenye makao makuu yake Vingunguti jijini Dar.

Leave a Comment