
MAHABUSU zaidi ya 20 waliokuwa wakishikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Maturubai, kilichopo Mbagala wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam wametoroka baada ya kumpiga askari kisha kuvunja lango la chumba cha mahabusu na kutokomea kusikojulikana.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea juzi Jumamosi, majira ya saa 1 usiku; “Waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo, si wale wenye kesi mbalimbali.”