
BAADA ya kukamilisha usajili wa straika mwenye mwili mkubwa, David Molinga, Kocha wa Namungo, Hemed Seleman Morocco, amesema mchezaji huyo ni mtambo wa mabao.
Morocco alisema yeye ndiye aliyependekeza jina la mchezaji huyo kwa kuwa tangu alivyoondoka Tanzania alikuwa akimfuatilia na akagundua kuwa alikuwa ameongezeka uwezo wake maradufu. Molinga alicheza Yanga msimu mmoja wa 2019/20, ametua Namungo baada ya kuondoka Zesco ya Zambia.

Akizungumza na Spoti Xtra, Morocco alisema: “Molinga ni mchezaji mzuri, nimemfuatilia tangu alipoondoka hapa.“Kule alikokwenda alikuwa ameongezeka ubora zaidi na amemaliza msimu akiwa na ubingwa wa ligi, naamini atatusaidia sana.”
Safu mpya ya ushambuliaji ya Namungo kwa msimu wa mwaka 2021/22 itaundwa David Molinga, Obrey Chirwa na Steven Sey.
ISSA LIPONDA, Dar es Salaam