
Watu watano wamefariki dunia kwenye ajali eneo la King’ori katika wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha leo Septemba 8, 2021 baada ya magari mawili ya mizigo kugongana uso kwa uso, waliofariki ni waliokuwemo kwenye Canter ambao ni abiria wawili na Dereva mmoja huku Dereva na Kondakta wa fuso pia wakifariki.