
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo akiuliza swali bungeni jijini Dodoma leo Septemba 8, 2021 kuhusu adha ya usafiri wa kivuko wanayoipata wananchi wa Kata ya Irunda na Kata ya Nyakaliro, katika vijiji vya Ntama, Mchangani na Kome wilayani Sengerema ambapo ameomba Serikali, amehoji ni lini serikali itapeleka kivuko kikubwa ili kuondoa kero hii kwa wananchi.