
JUMUIYA ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeisimamisha uanachama wa Guinea katika mkutano wa Viongozi wa Jumuiya kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya ambayo yalimwondoa Rais Alpha Conde madarakani .
Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mkutano uliofanywa kwa njia ya mtandao Jumatano, kwa mujibu na Reuters, uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry.
Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS alisema kuwa mapinduzi ya kijeshi yalikiuka makubaliano ya jumuiya hiyo kuhusu utawala bora.