Nyuma ya mafanikio ya kila mtu unayemuona amefanikiwa, ipo historia ya wapi alipoanzia na watu waliomshika mkono wakati anaanza safari yake ya mafanikio. Safari ya mafanikio ya msanii Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize, msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, haikuwa nyepesi na alipitia milima na mabonde kama mwenyewe anavyokiri mara kwa mara kupitia nyimbo zake na mahojiano anayoyafanya na vyombo mbalimbali vya habari.
Miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kumshika mkono Harmonize, ni Halima Abdul ambaye anaeleza kwamba yeye ndiye aliyempokea wakati anatoka kijijini Chitoholi, Tandahimba mkoani Mtwara kama alivyozungumza na waandishi wetu Richard Bukos na Issa Mnally. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx