Imelda Mtema
Haijakaa poa! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Fatuma Makame ‘Joanita’ anadaiwa kula kichapo ‘hevi’ kutoka kwa mumewe, usiku wa manane kwa madai kukutwa na ujumbe mfupi (SMS) zisizoeleweka kwenye simu yake.
Habari za kidaku zilieleza kwamba, wakati akila kichapo ilisikika sauti ya kilio kutoka nyumbani kwa Joanita na baada ya muda alionekana akikimbia kutoka nje ndipo walipomuhoji na kusema kuwa mumewe alikuwa akimpiga
. Alipobanwa na gazeti hili alidai kwamba ni mambo ya ndani kwake.