×

Beki Yanga Atuma Salamu Simba SC

BEKI wa kati wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amefunguka na kuelezea mipango yao kuelekea Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani zao, Simba itayopigwa wikiendi hii katika Dimba la Mkapa mkoani Dar.

 

Watani hawa wa jadi Yanga na Simba wamekutana mara nne kwa mwaka huu na hii ya Ngao ya Jamii itakuwa ya tano huku Yanga akiwa na rekodi nzuri kwa kushinda mara mbili na Simba moja pia wametoka sare mara moja.

 

Akizungumza na Championi Jumatano Mwamnyeto alisema: “Tumejipanga kama tunavyojipanga siku zote katika kila mechi ila tunajua mchezo huu utakuwa ni mgumu na siku zote haijawahi kuwa rahisi tukikutana na mtani.

 

“Imetuuma sana sisi kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa ila haina budi tumekubali matokeo tunaangalia mbele maana yameshapita tayari.”

 

Wikiendi iliyopita, Yanga iliondolewa hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa jumla ya mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria.

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave a Comment