
MWILI wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, William Ole Nasha unatarajiwa kuagwa kesho Bungeni Jijini Dodoma na kisha kusafirishwa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi siku ya Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhangama, mwili wa kiongozi huyo utaagwa kesho Bungeni saa 5 asubuhi kisha safari ya kuelekea Arusha itaanza.