×

Moto Waunguza Bweni na Darasa Sekondari ya Nyehunge

 

MOTO umezuka katika Shule ya Sekondari Nyehunge iliyoko katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza leo Jumatano, Septemba 29, 2021.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo moto huo umeunguza sehemu ya bweni na chumba kimoja cha darasa pamoja na mali za wanafunzi wa kidato cha tano na sita zilizokuwemo bwenini na darasani.

Hakuna madhara ya vifo ama majeruhi kwa wanafunzi, walimu au mtu yeyote ambayo yameripotiwa kutokana na moto huo. Tayari wanafunzi wamewahi kuokoa mali zao na kuziweka sehemu salama ili zizidhurike na moto huo.

 

Tayari Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kimeshafika eneo la tukio. Taarifa Zaidi tutakuletea hapa hapa.

 

Leave a Comment