×

Nape Akaribishwa Ofisi za Wizara Yake

1.Nape akizungumza mbele ya Wafanyakazi wa Wizara ya Habari.Waziri wa Wizara wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akizungumza mbele ya wafanyakazi wa wizara hiyo.2.Baadhi ya Wfanyakazi wa Wizara hiyo na wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo na wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.3.Nape akionesha hisia yake.Nape akionesha hisia ya jambo fulani.4.Hafla hiyo ikiendelea.Hafla hiyo ikiendelea.5.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari vijana utamaduni na michezo, Gabriel Ole Sante (aliyesimama) mbele ya Waziri na Naibu wake.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Gabriel Ole Sante (aliyesimama) mbele ya waziri na naibu wake akizungumza jambo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye, leo amekaribishwa na wafanyakazi wa wizara yake kwenye ofisi zao baada ya kuchaguliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa waziri wa wizara hiyo.

Nape amehudhuria hafla fupi ya kumkaribisha hii ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam, ambapo kwenye hafla hiyo amesema kuwa  wafanyakazi wa chini hadi ngazi za juu wanatakiwa kuwa na nidhamu na heshima kwa wakubwa na wadogo ili kuleta ufanisi na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.

Nape amesisitiza kupewa ushirikiano baina yake na naibu wake ili kuifanya wizara hiyo iwe wizara bora zaidi.

Aidha  amesema kuwa wizara hiyo imekuwa ikipatiwa bajeti ndogo ukilinganisha na ukubwa wa majukumu yake huku  akiahidi kuipigania katika vikao vya bajeti ili iongezwe na hivyo kutekeleza majukumu yake vilivyo.

Aliongeza kuwa atakuwa karibu na waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuwa mlezi badala ya mtawala ili kutatua changamoto zinazowakabili.

 NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment