×

Wananchi Brazil Waandamana Rais Aondolewe

MAELFU ya wananchi wa Brazil wameandamana tena nchini humo wakitaka rais wa nchi yao Jail Bolsonaro, aondolewe madarakani, kuhusiana na namna ambavyo anashughulikia janga la COVID-19 pamoja na masuala mengine.

 

Waandamanaji walikusanyika katika miji ya Rio de Janeiro, São Paulo, Brasilia na miji mingine kadhaa kama sehemu ya kampeni inayoungwa mkono na vyama kadhaa vya siasa za mrengo wa shoto na vyama vya wafanyakazi kumshinikiza Bolsonaro kuachia madaraka. Takriban watu 600,000 wamefariki nchini Brazil kutokana na janga la COVID-19.

 

Zaidi ya maombi 100 ya kutaka Bolsonaro atimuliwe madarakani yamewasilishwa katika mabaraza ya nchini humo dhidi ya rais huyo wa siasa za mrengo wa kulia. Lakini kiongozi wa bunge Arthur Lira amekataa kuchukua hatua yoyote.

 

Mahakama ya juu pia imeamuru chunguzi kadhaa dhidi ya Bolsonaro na washirika wake, ikiwemo tuhuma ya kueneza habari za uwongo.

 

Leave a Comment