×

Mpiga Picha Afuta Picha za Maharusi Baada ya Kunyimwa Chakula


KISA kimoja cha kushangaza kimewaacha watu midomo wazi baada ya mpiga picha mmoja aliyetofautiana na mwajiri wake wakati akipiga picha za harusi na kuamua kufuta picha zake zote ambazo alikuwa amempiga pamoja na mke wake.

 

Akitoa malalamishi yake kupitia mtandao wa Reddit, tuvuti maarufu ya Marekani, mpiga picha huyo alikuwa amekodishwa na rafiki yake ambaye alikuwa na sherehe ya harusi ili ampige picha za kumbukumbu ya tukio hilo adhimu.

 

Alisema bwana harusi huyo alimtafuta sababu ya gharama yake ya chini na baada ya kushawishiwa, cameraman huyo aliamua kuchukuwa tenda hiyo na kuwasili mapema katika harusi ya swahiba wake kuchapa kazi.

 

Akiwa amejihami na vifaa vyake, alianza kazi saa tano asubuhi na alikuwa ameratibiwa kumaliza kufikia saa moja usiku.

 

Katika hafla hiyo, wakati wa chakula uliwadia na kila mgeni alikuwa akipakuliwa. Mpiga picha huyo alijaribu kujumuika na wengine kwa chakula lakini alizuiwa na bwana harusi akihoji kuwa anatakiwa kupiga picha ya hafla nzima bila kusita wala kupumzika.

 

Alisema alikuwa amechoka sana, na hivyo alihitaji ni kupumzika angalau kupata kopo la maji ambalo nalo anadai alinyimwa.

 

Bwana harusi alimtishia kuwa hatamlipa iwapo atapumzika. “Nilimwambia bwana harusi kuwa nahitaji kupumzika kwa dakika 20 angalau kupata chakula na maji.

 

Lakini bwana harusi aliniambia kuwa natakana kuwa mpiga picha ama niondoke bila kulipwa,” aliandika mpiga picha huyo. Mpiga picha huyo alikasirika na kumuomba bwana harusi iwapo anaweza kufuta picha zote ambazo alikuwa amezipiga siku hiyo.

 

Bwana harusi alikubali na kisha mpiga picha huyo alifuta picha zote kabla ya kuondoka akiapa kutowahi kujihusha tena na hafla za bwana harusi huyo. Alisema pesa ambazo alikuwa anatazamia kulipwa zilikuwa kidogo na za kudunisha thamani yake.

Leave a Comment