×

Rais Samia Alivyowasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyowasili katika Viwanja vya Bunge na kukagua gwaride maalum kabla ya kuingia katika ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuhutubia na kufunga Bunge la 12 tarehe 27 Juni, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 27 Juni 2025, amewasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ambapo alipokelewa kwa heshima ya kitaifa na kukagua gwaride maalum.

Baada ya ukaguzi wa gwaride, Rais Samia alielekea katika Ukumbi wa Bunge ambako anahutubia kikao maalum cha Bunge na kufunga rasmi shughuli za Bunge la 12, kufuatia kuhitimishwa kwa muhula wake wa mwisho wa uendeshaji wa Bunge hilo.