×

Mrembo wa Diamond Avuruga Watu

 

MREMBO ambaye amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz anayetumia jina la Francia kwenye mitandao ya kijamii amevuruga watu siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa (birthday) ya jamaa huyo.

 

Francia ni mrembo mwenye umri wa miaka 20 aishie na wazazi wake, London nchini Uingereza, lakini mwenye asili ya Visiwa vya Madacascar ambaye amekuwa akizua gumzo kama lote baada ya kupostiwa na Diamond ambapo amemshushia bonge la ujumbe wa kuzaliwa na kuacha viulizo kwa watu.

 

Kupitia Instagram, Francia aliposti picha mbalimbali za Diamond kisha akamwandikia ujumbe huo huku akimuomba radhi kwamba hatakuwa naye kimwili katika kusherehekea siku yake hiyo, lakini wapo pamoja kiroho.

 

Kubwa lililoibua mshangao, ni baada ya mrembo huyo kumuita Diamond jina la Daddy ambalo hata Paula hulitumia kumuita Rayvanny ambaye ni mpenzi wake.

 

Hivi karibuni, kupitia Insta Story yake, Diamond alimposti ‘kitoto hicho’ akimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa hivyo kuwafanya wadukuzi kuanza kutafuta pa kuanzia ili kumjua zaidi.

 

Ni kweli mwenyewe anakiri kuwa na umri wa miaka 20 akimzidi Paula Kajala kwa mwaka mmoja. Katika maswali na majibu akiwa Insta Live, baadhi ya Wabongo walipita naye kumuuliza maswali kadha wa kadha.

 

Miongoni mwa maswali hayo ni kweli kwamba anampenda Diamond? Akajibu ndiyo na ni vizuri kupendana binadamu na binadamu. Anasema siyo yeye tu anayempenda Diamond bali hata mama yake na muda mwingi wanatumia kusikiliza muziki wake.

 

Hata hivyo, kati ya mambo anayojutia ni kutojua Kiswahili na hakuna kitu anachoficha juu yake na Diamond lakini anampenda Diamond na kamwe hawezi kumchukia Diamond kwani ndiye mtu anayempenda pekee hapa duniani.

 

Kubwa kuliko ni madai yake kuwa, bado hajatolewa usichana wake kwani hakuna mahali anapokimbilia kwani ndiyo kwanza ana umri wa miaka 20.

STORI; BAKARI MAHUNDU, DAR

Leave a Comment