×

UWT Makongo Wakabidhi Vifaa vya Usafi Mashuleni

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changanyikeni wakifurahia baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.

 

 

 

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT), Kata ya Makongo, umekabidhi vifaa kwaajili ya usafi wa vyoo katika shule mbalimbali za msingi na sekondari katika kata hiyo.

Viongozi wa msafara huo wakijadiliana jambo walipofika Sekondari ya Makongo Juu.

 

 

 

Akikabidhi vifaa hivyo, Jijini  Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo, Abriat Kivea, amesema  ni  katika kuadhimisha Wiki ya UWT ambayo inafikia kilele  hapo kesho.

Shule ya msingi Makongo Juu.

 

 

 

“Tuliona  tukabidhi vifaa hivi ili kuimarisha usafi kwa walimu na wanafunzi katika shule zote za serikali Kata ya Makongo,  UWT tunatambua  wajibu wetu katika suala zima la malezi kwa watoto, hivyo vifaa hivi vitawasaidia   kudumisha usafi shuleni,”anasema  Abriat.

 

 

 

Ameeleza kukabidhi vifaa hivyo  siyo mwisho bali  UWT Kata ya Makongo itaendelea kusimamia kikamilifu  malezi na kudumisha usafi shuleni.

 

 

 

“Tumekabidhi mifagio, sabuni za chooni, makopo na  kufanya usafi  katika vyoo vya walimu na  wanafunzi,”ameeleza.

 

 

 

Mwenyekiti huyo amedai UWT Kata ya Makongo,  waliona ni vema kusherehekea kwa njia tofauti Wiki ya UWT kwa kutoa vifaa  vya usafi badala ya kushiriki kufanya usafi pekee.

 

 

 

Katibu wa UWT wa Kata ya Makongo,  Deodata Komba, ametaja shule zilizonufaika kuwa ni  Shule  za Msingi Changanyikeni, Makongo  na Londa ambapo kwa upande wa Sekondari ni Makongo Juu. Wakipokea vifaa hivyo, walimu, wanafunzi na wajumbe wa kamati za shule hizo wameishukuru  UWT  Kata yaMakongo  na kudai  vifaa vimefika wakati muafaka ambapo  jamii inapambana na maambukizi ya   virusi  vya Uviko-19 .

 

 

 

“Katika mazingira kama haya yenye tishio la Uviko-19   usafi ni jambo la msingi mno kwa walimu na wanafunzi. Vifaa hivi  vitasaidia kudumisha usafi shuleni hivyo kuwakinga walimu na wanafunzi dhidi ya maambukizi  yakiwemo ya Uviko-19,”ameeleza  Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Changanyikeni, Elitia Sirro.

 

 

 

Mwalimu wa Shule ya Msingi Makongo, Joyce Kimaro amedai ,  UWT Makongo, imeonyesha ukomavu  hususan  wakati huu ambapo taifa linaongozwa na Rais  Samia Suluhu Hassan  na kitendo cha kukabidhi  vifaa hivyo kimewatia moyo.

 

 

Kilele  cha Maadhimisho ya Wiki ya UWT  kinafanyika kesho  ambapo katika Mkoa wa Dar es Salaam, maadhimisho hayo yanafanyika Wilayani Ubungo.

Leave a Comment