×

Exclusive: Fahyma Avunja Ukimya Kurudiana na Rayvanny

UKIAMBIWA utaje listi ya warembo wenye muonekano bomba Bongo, huwezi kuacha kumtaja mwanamitindo Faima Msenga almaarufu Fahyma ambaye amezaa na staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Fahyma amevunja ukimya kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kazi yake ya mitindo, maisha binafsi hasa ushiriki wa Rayvanny katika malezi ya mtoto wao wa kiume aitwaye Jaydany na mengineyo;

 

IJUMAA: Mambo vipi?

FAHYMA: Poapoa.

IJUMAA: Hivi ratiba yako ya siku ikoje?

FAHYMA: Mara nyingi ninapoamka asubuhi, kwanza kabisa nafanya mazoezi kwa sababu mimi always (kila mara) napenda kuonekana niko sex (navutia) kisha baada ya hapo nitaingia bafuni kuoga, nikimaliza ndiyo nitaenda mezani kwa ajili ya kupata matunda kwa sababu mimi siyo mpenzi wa chai sana.

 

IJUMAA: Asilimia kubwa ya watu huwa wanaamini kuwa mtu asiyependa chai, basi anatumia kilevi, hii kwako imekaaje?

 

FAHYMA: Binafsi nipo tofauti kwa sababu mimi mchana na asubuhi nakula matunda ila ikifika usiku ndiyo naweza kula viazi na maziwa kwa sababu napenda kuonekana na mwili mzuri, sasa ukiwa unakulakula ovyo maugali, chipsi, sijui na vitu gani, huwezi kuwa hivyo, ndiyo maana mimi tayari nimezaa, lakini bado nina mwili mzuri.

 

IJUMAA: Kitu gani ukifanya kwenye maisha yako una-enjoy kupita maelezo?

FAHYMA: Aisee napenda kufanya shopping ya nguo, viatu, pochi, make-up na vitu vingine; yaani hapo ndiyo roho yangu inakuwa nyeupe.

IJUMAA: Huwa unafanya shopping kwa wiki mara ngapi?

 

FAHYMA: Mara nyingi huwa nafanya shopping kwa wiki mara tatu, lakini kwa vitu kama cheni, hereni, bangili na vitu vingine vidogovidogo kama hivyo naweza kufanya kila siku.

IJUMAA: Mastaa wengi ukiwauliza wanasema shopping zao hupenda kufanyia nje ya nchi hasa Dubai vipi kwa upande wako?

 

FAHYMA: Mara nyingi huwa nafanyia online (mtandaoni) kwa sababu napenda kuwa unique (wa kipekee), sipendi kuvaa nguo ambayo kila mtu anayo hivyo huwa naagiza kisha ananiletea, lakini viatu vyangu huwa napenda kununua Tin Shoes kutoka UK (Uingereza).

 

IJUMAA: Umesema hupendi kuvaa vitu ambavyo na wengine wanavyo, lakini una skendo ya kuiga mavazi ya mastaa wakubwa wa nje ya nchi kama Kim Kardashian, Beyonce na wengineo; hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki wakuone kama umeishiwa ubunifu.

 

FAHYMA: Hakuna ambaye haigi, unajua ukitaka kumuiga mtu, basi hakikisha umemfunika kabisa, sikatai kuwa ndiyo huwa napenda kuwaiga, lakini ninyi wenyewe mnaona napendeza pengine hata kuwazidi hivyo ndivyo inavyotakiwa.

IJUMAA: Kuna mtu ambaye huwa anakudizainia mavazi?

 

FAHYMA: Kiukweli huwa napenda kujidizainia mwenyewe.

IJUMAA: Huwa unavaa nguo za mtumba?

 

FAHYMA: Sana tu; yaani navaa nguo yoyote iwe ya mtumba au ya dukani hivyo hata nikute nguo inauzwa bei gani kama nimeipenda, nitainunua tu, mfano nikikuta nguo inauzwa 3,000 na ni nzuri, nitanunua na hata kama nikikuta nguo inauzwa zaidi ya shilingi milioni 5.

 

IJUMAA: Ni kitu gani huwa unakipenda ukiwa na mwanaume wako?

FAHYMA: Napenda awe ananukia pafyumu muda wote; yaani akiwa anapendeza mimi hoi.

IJUMAA: Ukiwa na msongo huwa unapenda kufanya nini ili kupoteza mawazo ulionayo?

FAHYMA: Nikiwa na msongo napenda kulala tu na asinisumbue mtu yeyote hadi nitakapoamka.

 

IJUMAA: Msanii gani wa ndani na nje ya Bongo ambaye huwa unamtazama kama mfano wa kuigwa?

FAHYMA: Jacqueline Mengi (K-Lyyn), nampenda na ni mfano mzuri wa kuigwa, kwa nje ni Kim Kardashian.

IJUMAA: Fahyma ni mwanamke wa aina gani kwa watu ambao wamezoea kukuona mitandaoni?

 

FAHYMA: Ni msichana mwenye roho nzuri, mwepesi kuguswa na matatizo ya watu na kuwasaidia, napenda fasheni na ni mtu ambaye hata usemeje mambo mabaya kuhusu mimi huwa sijali.

IJUMAA: Unapenda kuwa na marafiki wa aina gani?

 

FAHYMA: Kwanza sina marafiki, halafu sipendi kuwa na marafiki kwa sababu ukiwa nao ndipo matatizo yanapoanzia hivyo marafiki zangu ni wale ambao wameni-follow Instagram na wanao-comment kwenye akaunti yangu basi.

IJUMAA: Vipi Rayvanny anashiriki katika malezi ya mtoto wenu?

 

FAHYMA: Mtoto wangu hakuna anachokosa kwa sababu anatuona wazazi wake wote.

IJUMAA: Kwa nini haujabadili jina lako la Fahyvanny kwenye Instagram?

FAHYMA: Kwanza watu watambue kuwa jina langu Instagram limeshakuwa verified, pia sioni umuhimu wa mimi kulibadili, halafu hata nikibadilisha haina maana.

 

IJUMAA: Ulisema huwezi kuachwa kwa sababu wewe ni mtoto wa Kitanga, lakini umeachwa na mwanaume yupo na Paula, hilo unalizungumziaje?

FAHYMA: Sidhani kama mimi nilisema hayo maneno.

IJUMAA: Unazungumzia voice note au sauti zilizosambaa kuwa unamfuatilia Paula?

FAHYMA: Nilizisikia, lakini hazikuwa za kwangu.

MAKALA: MEMORISE RICHARD, BONGO

Leave a Comment