Uongozi wa Bricoleur Company kutoka Japan na baadhi ya watu wa Kikundi cha Tingatinga Arts wakiwa meza kuu.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, Bricoleur Company, Shoji Tsuchiya, Yu Shiran na Mwenyekiti wa Kikundi cha Tingatinga, Zachi Chimwanda.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi hao wakishikilia baadhi ya vibao vilivyochorwa picha tofauti.
Kiongozi kutoka Bricoleur Campany, Shoji Tsuchiya (kushoto) na Zachi Chimwanda wakiweka saini zao katika mikataba.
Viongozi hao wakibadilishana mikataba hiyo.
CHAMA cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), kimewataka wasaniii wa sanaa ya uchoraji kupanua soko la mikataba ya sanaa ili kuweze kuwa ya kimataifa.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) katika mkutano wa kusaini mkataba kati ya Kikundi cha Sanaa ya Uchoraji cha ‘ Tingatinga Arts’ na Kampuni ya Bricoleur kutoka Japan, Afisa mtendaji wa chama hicho, Doreen A. Sinare amesema wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu na kutafuta soko la nje maana wadau wengi wa sanaa ya uchoraji hutokea nje ya nchi.
Sinare amesema kuwa wasanii wa sanaa ya uchoraji wanapaswa kutazama mfano wa utendaji kazi wa kikundi hicho katika soko la kimataifa ndani ya mkataba huo wa miaka mitano uliosainiwa na Mwenyekiti wa Kikundi cha Tingatinga, Zachi Chimwanda.
Alifafamua kwa kusema, mkataba huo unapaswa kuugwa mkono na wasanii kwa kuangalia wadau hao na kupima mwendendo wake ili nao kutafuta soko zaidi na kuitangaza Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema kupitia mkataba huo wasanii wa sanaa za uchoraji wa Tingatinga watanufaika kujitangaza na kujipatia kipato na kupata maendeleo kupitia sanaa hiyo.
NA DENIS MTIMA/GPL