×

Kifo cha Ole Nasha, NEC Yatangaza Uchaguzi Ngorongoro

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo Jumatatu, Oktoba 18, 2021 imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, unaotarajiwa kufanyika Desemba 11, 2021 kuziba nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, William Ole Nasha.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo, Dk. Wilson Mahera inaeleza kuwa zoezi la kuchukua fomu za uteuzi litaanza Novemba 17 hadi Novemba 15,2021 utakapofanyika uteuzi wa wagombea ambapo kampeni zinatarajiwa kuanza Novemba 16, mwaka huu.

 

Uchaguzi huo utaenda sambamba na uchaguzi wa diwani katika Kata ya Naumbu, Mtwara kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Rashid Aderehemani wa CUF aliyefariki dunia Agosti 29, 2021.

Leave a Comment