
SAYANSI inasitasita kuamini juu ya uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito huku akiwa na ujauzito mwingine tayari.
Lakini visa vilivyowatokea baadhi ya wanawake kujikuta wakijifungua watoto waliopishana umri vimewaacha wataalam midomo wazi na kusema “inawezekana.”
Hivi karibuni nchini Australia mwanamke anayeitwa Kate Hill alijifungua watoto Charlotte na Olivia ambao walikuwa wamepishana umri.
Aprili mwaka huu, mwanamke Rebecca Roberts, raia wa Marekani alijifungua mapacha ambao walikuwa wametofautiana umri kwa wiki tatu.
Hii inamaanisha kwamba, mimba ya kwanza ilitungwa na baada ya wiki tatu ikatungwa nyingine jambo ambalo daktari wa mwanamke huyo aitwaye David Walker kutoka hospitali ya Royal United anasema ni tukio linalofikirisha.
Ingawa mtandao wa healthline.com unataja mambo matatu ambayo humfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito juu ya ujauzito likiwemo lile la mji wa uzazi kuzuia njia baada ya yai kurutubishwa lakini visa zaidi ya kumi vilivyojitokea duniani vimetosha kulifanya jambo hilo liaminike kuwepo na kupewa jina la ‘superfecundation’.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa mapacha waliopatikana kwa utungaji wa mimba mbili tofauti huweza kuishi katika mifuko tofauti huku kila mmoja ukijitwalia damu kwa njia yake.
Unaweza kukopi link hii kusoma moja ya visa vya mwanamke kujifungua mapacha waliotokana na mimba zilizotunga nyakati tofauti.
Soma zaidi hapa
@manyota_rich