×

Watu 690 Wameuawa Simiyu

TAARIFA zinaeleza kwamba watu 690 wameripotiwa kuuawa kwa kukatwa mapanga katika mkoa wa Simiyu, wengi wao wakiwa ni wanawake.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu (RCO), Mrakibu Mwandamizi wa jeshi hilo, Israel Makongo, ambaye amewaambia wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani humo kuwa, mauaji ya watu hao yamefanyika kwa kipindi ha miaka tisa kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka huu 2021.

 

“Mauaji haya ni wastani wa watu 37 kwa kila mwaka, lakini ukiangalia wanaouawa zaidi ni wanawake wenye umri kati ya miaka 40 hadi 80. Sababu ni zinazotajwa ni dhuluma, pengine mtu anataka kurithi mashamba, ng’ombe ama mali, wengine ni wivu wa mapenzi,” amesema Makongo.

 

Aidha, Makongo amewataka viongozi hao wa Halmashauri, Madiwani, wenyeviti wa vijijini kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na amani katika maeneo yao.

Leave a Comment