×

Wasanii Hawa Wajitafakari Sana Kuhusu Mashairi Yao

Umeisikia hii ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas ambaye ameamua kuvunja ukimya na kujibu swali aliloulizwa iwapo kwenye Playlist yake ana nyimbo za marapa Rroma Mkatoliki na Nay wa Miotego, na kama anazo ni zipi.

 

Akijibu swali, Dkt. Abbas amedai hana kumbukumbu ni nyimbo ngapi anazo au anazipenda kutoka kwa wasanii hao lakini anapenda wimbo mmoja wa Roma unaitwa Zimbabwe. Ameyazungumza haya akiwa Bagamoyo kwenye tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni.

 

Aidha, Dkt. Abbas amewataka wasanii hao wajitafakari mashairi wanayoandika kama wanataka kuwa walalamishi tu (wanaharakati) ama wanamuziki wanaotaka kwenda mbele na kuendeleza sanaa zao.

 

Dkt. Abbas amesema pia kwamba iwapo msanii atakuwa na nyimbo zenye maudhui mabovu na yenye kuikashifu serikali basi wasahau kuitwa kwenye matamasha ya serikali pia.

Leave a Comment