×

Kiba, Amina Wawafokea Mashabiki!

WANATUFOKEA! Ndivyo wanavyosema wajumbe kwenye mitandao ya kijamii baada ya mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh ‘King Kiba’ kuonekana kwenye mahaba ya mwendokasi na mkewe, Amina Khaleef.

 

Kiba anatajwa kuwa ni staa anayependa kuweka mambo yake ya kifamilia kuwa siri, jambo ambalo limekuwa likiibua tetesi kuwa, huwenda ndoa yake na Amina imevunjika.

 

Tangu kuibuka kwa tetesi hizo mapema Februari, mwaka huu ambapo Kiba alizikanusha, jamaa huyo hakuwahi kuonekana katika picha moja na Amina.

 

Lakini wikiendi iliyopita, Kiba aliachia picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na Amina kwenye pozi za ‘mtafi cha wapi sura zenu’. “

 

Arusha I’m in Town! Tukutane Viwanja vya Relini (Arusha) kuanzia saa 6:00 mchana kumpa support ndugu yangu, rafi ki yangu, Mrisho Gambo na Chama cha Mapinduzi (CCM),” aliandika Kiba kwenye picha hizo zilizosambaa fasta kama moto wa kifuu ambapo alikuwa Arusha kwa ajili ya shoo ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi za mgombea wa Arusha-Mjini kwa tiketi ya CCM, Mrisho Gambo.

 

Ikumbukwe kwamba, Kiba alifunga ndoa na mkewe asubuhi ya Aprili 19, 2018 kule jijini mjini Mombasa nchini Kenya na wamejaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Keyaan.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR.

Leave a Comment