
Fredy Kapala shahidi wa tano wa upande wa Jamhuri katika kesi ya tuhumza za ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ametoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Kapala aliyejitambulisha kuwa ni mwanasheria wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo ametoa ushahidi huo leo Jumanne Novemba2, 2021.
Ifuatayo ni sehemu ya ushahidi:
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kabla hatuja Anza Maswali ya Dodoso nilikuwa naomba Mahakama itambue Uwepo wa Wakili Mwenzangu Nashon Nkungu.
Jaji anaandika Kidogo..
Mtobesya: nilikuwa naongea na wenzangu kama Tutapata mapumziko ya Afya lakini naomba Niulize mimi Japo kwa nusu saa tu baada ya Hapa Nina kesi mahakama ya Rufani nitaacha wenzangu waendelee
Jaji: itakuwa vizuri ukituma Dakika 20
Mtobesya: Shahidi Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali ulielezea kwa urefu sana Namna ambavyo Mnafanya kulinda Mfumo wenu Pamoja na Server, Je Ni sahihi
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Lakini Hukuiambia Mahakama Mpaka Wakati Unatoa Taarifa hapakuwa pamefanyika Audit ya namna gani na Kwamba System Ilikuwa Vizuri
Shahidi: Sahihi
Mtobesya: sikusikia Ulisema Kwamba Servers zinaweza kuingiliwa na Mahakama
Shahidi (Tigo): Sahihi
Mtobesya: Wakati Jaji akiandika elezea HACKERS ni Watu gani
Shahidi (Tigo): ni Wataalamu wa Mitandao ambao wanasoma Mfumo au Wanakuwa wanamfahamu Mfumo na Wanatabia ya kujaribu Kuingia Kwenye Mfumo, Kuchukua ama Kuharibu Taarifa ama Mfumo Wenyewe
Mtobesya Nitakuwa sahihi nikisema wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Hukusema kama palikuwa na Possibility za Hackers Kuingia Kwenye Mfumo
Shahidi (Tigo): Ndiyo Sikusema
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Nikisema Hackers Wanauwezo wa Kuingia na Kucheza na Taarifa za READ ONLY kama alivyokuwa anakuongoza Wakili wa Serikali
Shahidi (Tigo): Ndiyo Uwezekano Upo
Mtobesya: Ofisi ya Tigo ulisema ni nini
Shahidi (Tigo): Jina la Kibiashara
Mtobesya: Ofisini kwenu kuna wanasheria Wangapi
Shahidi (Tigo): Kwa Ujumla au Legal Department.?
Mtobesya: Legal Department
Shahidi (Tigo): Watatu
Mtobesya: Nilisikia Ulisema wanaweza Kuingia Kwenye Mfumo ni watu wa Mantainance na Audit, Je Kuna lolote Umetoa lenye Jina lako kwamba wewe ndiyo ulishughulikia Taarifa hizi
Shahidi (Tigo): Mbali na Barua kwa kweli Hakuna
Mtobesya: na Barua pia haina Jina
Shahidi (Tigo): Ndiyo haina Jina
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Barua ithibitishe hiyo
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Nikisema Kwenye Taarifa ya KYC (KNOW YOUR CLIENT) haihitaji Barua za Utambulisho kama Serikali za Mitaa
Shahidi (Tigo): Hapana haihitaji
Mtobesya: tuweke Record sawa kwa hiyo hata Photocopy Ya Kitambulisho Cha NIDA haihitajiki
Shahidi: NI Scanned ID
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi nikisema KYC inatakiwa iambatane na hiyo Image ya Kitambulisho Cha NIDA
Shahidi (Tigo): Siyo lazima
Mtobesya: Nitakuwa sasa Kwenye Kielelezo namba 09 Cha Mtu Uliye Sema ni Freeman Mbowe Taarifa zake Hazipo
Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 09
Mtobesya: Nionyeshe Jina la Mtumishi aliyesajili
Shahidi (Tigo): Siyo Mtumishi ni Mtu Mwenye Device
Mtobesya: Ndiyo huyo huyo Nionyeshe Jina lake
Shahidi (Tigo): Halipo
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema hata Mtu aliye sajili haionekani alisajilia wapi?
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mtobesya: Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa kwanza Naomba Kumaliza
Mallya: Shahidi wewe ni Wakili siyo
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Umekuwa Admitted Kwenye Bar Mwaka gani
Shahidi (Tigo): 2013
Mallya: Tigo Umeajiliwa lini
Shahidi (Tigo): 2012
Mallya: na Uliajiriwa Department gani
Shahidi (Tigo): Legal Department
Mallya: Ulitaja Department Zingine Kwenye Ushahidi wako
Shahidi (Tigo): Ndiyo Kama IT Security
Mallya Kazi zake..?
Shahidi (Tigo): Ulinzi wa Taarifa za Mfumo na Taarifa zote zinazoshughulika na wateja
Mallya: hiyo Department ya Security Bwana Yahaya Zahoro ndiye anayeshughulikia Taarifa kama hizi
Shahidi (Tigo): Yeye ni Internal Investgation Officer
Mallya: yeye ndiye anaye Shughulikia Maswala kama haya
Shahidi (Tigo): Siyo haya
Mallya: kuna Department inayoshughulika na Masuala External Investigation
Shahidi (Tigo): hatuna, hiyo labda ni Polisi na Serikali
Mallya: Ulizungumza lolote kuhusu Telepin
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulisema ni nini
Shahidi (Tigo): Mfumo Mmoja Ulikuja Kure place Mwingine
Mallya: Upi Ulianza
Shahidi (Tigo): Ulianza CONVIVER Ukaja Telepin
Mallya: kwanini waliondoa CONVIVER
Shahidi (Tigo): Kwa sababu ya Mabadiliko ya muda na Technology
Mallya: Wakati Unatoa Exhibit P8 suala la Miamala ya Fedha Ulielezea Mahakama Kwamba Ulizungumza Kutoka Kwenye Software gani
Shahidi: Screen Server
Mallya: wakati Unaona hizi Taarifa Ulisema Umetumia Mechanism Gani Kugenerate hii Print Out
Shahidi: Nilichagua Option ya Kuprint
Mallya: Kwanini Ulichagua Kwanini Uliacha Option Ya Screenshort ukaamua Kuprint
Shahidi (Tigo) Ilikuwa ishu ya Choice tu
Mallya: Kuhusiana na Jina lako Mwanzoni palikuwa na Maombi ya Kubadili Kutoka Frank Kwenda FREDY,
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mallya: Je Kapala ni R au L Mwishoni
Shahidi (Tigo): NI L Mwisho
Mallya: Kwa hiyo huyu Kapara siyo wewe
Shahidi (Tigo): Inaweza Kuwa wamechanganya
Mallya: Wewe ni Wakili unajua Madhara ya kukosewa Jina
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Life cycle ya Simu Card unaweza Kupata Wapi
Shahidi (Tigo): SQL server
Mallya: Mimi ninao Ushahidi inapatikana Kwenye SMAP
Shahidi (Tigo): Ndiyo inapatikana pia
Mallya: Unababilisha Jibu eeh!
Shahidi (Tigo): Hapana Kote unaweza Kupata Kote
Mallya: Taarifa uliyoileta KYC ni Taarifa Accuracy?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Unataka Mahakama Ikueleweje ukisema Accuracy
Shahidi: Nimezipata Kwa Njia iliyokamilika sina Wasiwasi nazo
Mallya: Hapo Kuna Mpangilio wa Taarifa Je umeelezea Sababu Ya Kupanga hivi
Shahidi: Hapana
Mallya: Kuna City imeandikwa Kilimanjaro Je Ulimwambia Jaji hiyo Kilimanjaro City Unaifahamu
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: hiyo Kilimanjaro City unaifahamu
Shahidi (Tigo): Hakuna Kilimanjaro City
Mallya: Kuna District inaitwa Kinondoni, Je huko Kilimanjaro inaweza kuwa District ya Kinondoni?
Shahidi (Tigo): SAMAHANI KIDOGO
Mallya: NISHAKUSAMEHE
Shahidi (Tigo): RUDIA SWALI
Mallya: Kuna City ya Kilimanjaro, kuna District ya Kinondoni
Shahidi (Tigo): hakuna
Mallya: Kuna sehemu hapo imeandikwa Region, Region gani?
Shahidi ( @Tigo_TZ ): Kimyaaaaaaaaaa
Mallya: Je huko Dodoma Kuna Sehemu Inaitwa Kilimanjaro City?
Shahidi (Tigo): Hakuna
Mallya: Unasemaje Kuhusu hizo Taarifa
Shahidi (Tigo): Kuna Taarifa ambazo zipo NIDA so Ukiweka Kidogo Nauliza Mfumo wa NIDA, Mtu Mwenye Jina hili na Fingerprints hizi Zina Match
Zinasoma anaitwa nani, na Taarifa zake zote zinakuja Kama hazipo zinakuja Kuhuishwa siyo Za NIDA Kama hazipo ni za kwetu sisi
Mallya: kama Taarifa hakuna Je Freeman Mbowe alijisajili Mwenyewe
Shahidi: Nahisi Wakili hatuelewani katika hili, Nilisha Sema Kama Taarifa zilizotakiwa Kuchukuliwa NIDA kama Hawana Sisi tulipaswa kuchukua NIDA
Mallya: Kielelezo 09 kimetoka kwenu au NIDA
Shahidi: kwetu
Mallya: Kwa hiyo Hiyo Mitambo ya kuprint ipo NIDA au Ofisini Kwenu
Shahidi (Tigo): Ofisini Kwetu
Mallya: Aliyemsajili Mbowe nani kama Kweli Mbowe ana namba ya Tigo
Shahidi (Tigo): Simjui
Mallya: Kwanini humjui
Shahidi (Tigo): Sababu Kwenye Taarifa hiyo Sijamuona
Mallya: Nitakuwa sahihi Nikisema Taarifa Yenu Haipo Kamili nitakuwa Sahihi
Shahidi (Tigo): Haupo Sahihi
Mallya: pale Ofisini Kuna Department ya Tigo Pesa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulizungumzia kuhusu Tigo Pesa Department.?
Shahidi (Tigo): Siku zungumzia
Martin Maranja Masese @IAMartin_ · 2h Mallya: Mimi siiijui kama namba ni ya Freeman Mbowe au Lah, lakini hebu niambie Pale Kwenu Kuna Kitengo cha Business to Business kama Post paid
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulizungumzia Hiyo
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Hii namna ya Kujibu Mabarua ni Standard Form au Kila Barua na namna yake
Shahidi (Tigo): NI Standard Form
Mallya: Lengo la Kuweka ENEO la Kujaza Kosa la Mteja wenu wanalomchunguza nalo
Shahidi (Tigo): NI Format ya Kuweka Kosa wanalo mchunguza nalo
Mallya: Je Polisi Wakitaka Uwape Taarifa ya kuchunguza Girl Friend wake we utatoa taarifa
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya Je wewe Ulipata Kuuliza Wana mtuhumu Kwa Makosa gani
Shahidi (Tigo): Hapana Sikuuliza
Mallya: Kwa hiyo wewe Ukatoa Taarifa hata akama Mtu anataka Kujua namtumia pesa Mpenzi wake
Shahidi (Tigo): Siyo Utaratibu wangu wa Kazi
Mallya: Kwa hiyo nyie Tigo manataka Kutuambia Kuwa Polisi Wakitaka Taarifa hata kama hawana Kosa la Kuchunguza Mtawapa
Shahidi (Tigo): Siyo lazima pawe na kosa la Jinai, Kazi yangu ni kuona Kama Wamekidhi vigezo
Mallya: Ni Mara yako ya Kwanza Kupata Barua Kutoka Forensic Bureau
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Kwani Forensic Bureau Wanahusika na masuala ya ndoa na matunzo ya watoto?
Shahidi (Tigo): Mimi naangalia namba na kutoa taarifa
Mallya: Hukuona umuhimu wa kujua kosa..?
Shahidi ( @Tigo_TZ ): Siyo kazi yangu kujua makosa
Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Jaji; anaandika Kidogo
Jaji; Tutaenda break Dakika Ngapi
Kibatala: Ngoja tushauriane
Jaji; Sawa
Wakili wa Serikali; Tumekubaliana na Wenzetu Tubreak Kwa Dakika 40 turudi saa 08 kamili
Jaji; basi tunabreaka kwa Dakika 40 tutarudi Saa 08 kamili, Naomba tutunze Muda
Mallya: Je KAPALA ni R au L Mwishoni?
Shahidi: NI L Mwisho
Mallya: Kwa hiyo huyu KAPARA siyo wewe?
Shahidi: Inaweza Kuwa wamechanganya
Mallya: Wewe ni Wakili unajua madhara ya kukosewa Jina?
Shahidi: Ndiyo
Jaji ameingia tena
Kesi inatajwa tena.
Kibatala: Naomba Wakili Dickson Matata Kwa Ruhusa yako aingizwe Katika column
Nilimuombea Ruhusa Kwamba atachelelewa na Kwa Sasa ameshafika
Namualika Wakili wa Mshtakiwa wa 03 aweze Kuuliza Maswali ya Dodoso
Matata: Nilikusikia Kwamba Kwenye Kitengo Cha Sheria Mpo watatu
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Ukusema nani Mkuu wa Idara Yenu
Matata: Na Hukusema Wewe licha ya Kuwa Mwanasheria Ni Mkuu wa Idara, Kweli siyo kweli
Shahidi (Tigo) +/ Siyo Kweli
Matata: licha ya Kuwa Wewe Mwanasheria Hukusema Wewe unanafasi gani Nyingine
Shahidi: Siyo Kweli
Matata Ikae hivyo hivyo Mheshimiwa Jaji
Matata: wewe Ndiyo umepokea Barua, wewe Ndiyo umeprint Taarifa, na Wewe Ndiyo Umepeleka Majibu Polisi
Shahidi (Tigo): Sijaelewa
Matata: Wewe Ndiyo ulipokea Barua
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: wewe Ndiyo uliandika Barua
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Nitakuwa sahihi nikisema wewe Ulifanya Kila Kitu Kwa Niaba ya Tigo
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Ulielezea Mahakama Kwamba Kwanini Wenzio 3 hawakushiriki katika hiyo kazi
Shahidi (Tigo): Siyo kweli
Matata: kampuni yenu mnasera ya Usiri?
Shahidi (Tigo): Upo sahihi
Matata: ambapo Mawasiliano ya mteja yanakuja ni Siri kati ya Mteja na Nyinyi
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: Kwamba nitakusa sahihi nikisema Moja ya Sababu Ya Kuvunja Usiri ni endapo panahitajika Kufanya Uchunguzi Kwa VYOMBO Vya Uchunguzi
Shahidi (Tigo) Sahihi
Matata: Na Utoaji huo Wa Taarifa unalindwa na Sheria
Matata: Na wewe ni Mwanasheria
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Na Mimi nimekusikia Mtatoa Taarifa Endapo Mtaombwa au Kwa Amri ya mahakama
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: Kwa kuzingatia Umuhimu wa Usiri wa mteja Nisomee Kifungu cha 34 cha Sheria Ya a Makosa ya Mtandao
Shahidi (Tigo): 34(i) Disclosure of Data………
Matata: Utakubaliana na Mimi kwamba Pale panapohitajika Taarifa Ya Uchunguzi Police ambaye ni Ofisa anaweza Kuomba Taarifa Kwenu
Shahidi (Tigo): Hapo anaongelea Ongoing Trafficking Data siyo Stored Data
Matata: Mh Jaji naomba Kielelezo
Matata: hiyo Barua Wametumia Kifungu gani
Shahidi (Tigo): Kifungu cha 34 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao
Matata: Na Mimi nimekuuliza Usome Kifungu gani
Shahidi (Tigo): Kifungu hicho hicho cha 34
Matata: Kwa hiyo utakubaliana na Mimi wewe Umeombwa Kitu Kingine na wewe Ukatoa Kitu Kingine
Matata: Kwa Mujibu wa Maelezo yako walitaka Uwapo Data Trafficking Ya Siku hiyo Siyo Stored Data
Matata: naomba Unisomee hapa
Shahidi kutoka @Tigo_TZ anasoma kwa sauti sheria tajwa
Matata: Utakubaliana na Mimi kwamba Kama Mtu ameombwa Taarifa na akakataa na Yule Police Officer alitakiwa kwenda Mahakamani Kuomba Court Order
Shahidi (Tigo): NI sahihi
Matata: Naomba Unionyeshe Kwenye hii Barua ni wapi Pameonyeshwa Kosa Kwenye hiyo Barua ambapo hiyo namba Inatuhumiwa kwenye Kosa la Jinai
Shahidi: Hakuna
Matata: Kuna Kosa Umeandika hapa Wakati Unajibu Barua hii Kuhusiana na Uchunguzi
Shahidi (Tigo): Kuna Dash Hakuna Kosa
Matata: Kwa hiyo Hakuna Kosa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Pamoja na Barua kuja Bila Kutaja Kosa na Wewe Ukatoa Taarifa hiyo bila Kutaja Kosa kama Inavyosema katika Kifungu 34
Je Hukuona hilo ni Jambo lisilostahili ili uwakatalie Waende Mahakamani Kulinda Usiri wa wateja wenu
Shahidi (Tigo): Hapakuwa na Haja hiyo
Matata: Kwa hiyo Polisi Wakikuandikia Barua ya Kutaka Taarifa Bila Kukutajia Makosa
Shahidi (Tigo): Nitampa
Matata: Kwenye kampuni yenu haitaji la Kutuma Meseji au Kupiga Simu Kwenu ni Kosa
Shahidi (Tigo): Hapana Siyo Kosa
Jaji: wakili wa mshtakiwa namba 4
Kibatala: Nyie Kama @Tigo_TZ MIC Tanzania Ltd Priority ni nini, USIRI wa MTEJA au Kufuata MASHARTI ya POLISI?
Shahidi (Tigo): Tuseme COMPLIANCE na SIRI za MTEJA
Kibatala: Sawa tuweke hivyo Kwenu Kipaumbele ni nini?
Shahidi (Tigo): COMPLIANCE
Kibatala Unafahamu Kuwa Mtu uliyemtolea Ushahidi Kama Freeman Mbowe Kuwa ni Kiongozi wa Chadema kama Kiongozi wa Chama Cha Upinzani
Shahidi (Tigo): Simfahamu
Kibatala: Umekuwa Wakili tangu lini
Shahidi (Tigo): 2013
Kibatala: Bado unataka tukubali kuwa humfahamu Freeman Mbowe kama Kiongozi wa Chadema, chama kikuu cha upinzani Tanzania?
Shahidi (Tigo): Ndiyo sifahamu, Wapo wengi
Kibatala: Barua ilisema Kwamba iwe ni Siri sana Mteja asijue?
Shahidi (Tigo): Haiku Sema hivyo
Kibatala: Ulimtaarifu Mteja Mwenyewe kwamba Kuna Taarifa zako za Kiuchunguzi zinahitajika
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kama Kampuni Mlichukua Hatua yoyote ya Kumlinda Mteja Kwa kwenda Mahakamani Kupinga au Kuandika Barua kwenda TCRA, Mlichukua hatua kama hiyo
Shahidi: Hapana
Kibatala: mlichukua hatua gani kumlinda mteja
Shahidi (Tigo): Hiyo siyo kazi yetu, Hakuna hatua tuliyoichukua kumlinda mteja
Kibatala: Mnafahamu Angalau kuwa Kuna Tasisi Mbili angalau zinahusika Kulinda Maslahi ya Mteja
Shahidi (Tigo): Ndiyo nazifahamu
Kibatala: Zitaje
Shahidi (Tigo): TCRA na FCC
Kibatala: Hakuna Polisi Wana abuse power zao
Shahidi (Tigo): Sifahamu
Kibatala: Barua Yako uliyoitoa Mahakamani, Je Mahakama Ikitaka Kujua Kuwa nini wewe Mmiliki wa Barua, Ina angalia Wapi
Shahidi: Kielelezo namba p6
Kibatala: Msaidie Mheshimiwa Jaji akiangalia Wapi ataona Barua hii Umesaini wewe FREDY Kapala
Shahidi (Tigo): Barua Yenyewe Ilipotoka ni MIC Tanzania Ltd na Pia Nimesema ni Saini Yangu
Kibatala: Mimi nasema Hakuna Mahala Popote pale ambapo Pana Majina yako Katika Kielelezo namba p6
Shahidi (Tigo): Ndiyo Hakuna Majina
Kibatala: Je Uliongozwa na Wakili wa Serikali Kutoa Nyaraka Nyingine Kufanya Ulinganifu kwamba hii ni Saini yako
Shahidi (Tigo): Sikuyatoa
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa Hatuna sehemu ya Kulinganisha Signature Yako
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Tuchukulie Kwamba Barua Iliandikwa na Polisi na wewe hii ni Saini Yako, Je ni wapi Mheshimiwa Jaji akiangalia anaweza Kuona Barua hii Ilipita kwa Wengine Tigo kwamba Ufanye kama kwa Ku’ minute
Shahidi (Tigo): Sijaelewa
Kibatala: Unafahamu Kuwa baadhi ya Ofisi Barua inatembea na kupelekwa kwa Mhusika baada ya Kupita kwa wengine
Ulimwambia Jaji kama Nyie Tigo hamna Utaratibu huu
Shahidi: Siku Mwambia
Kibatala: Unakubaliana Barua Yako ya Tarehe 02 Haielei hewani Ndiyo Maana Inaviambatanishi
Shahidi (Tigo) Ningeweza Kujibu Lolote
Kibatala: Taja Kwa Nguvu hiyo kumbukumbu namba ya katika Barua ya Polisi Kama kiambatanisho p6
Kibatala: Msomee Jaji Sasa Nyaraka ambayo wewe umenukuu kwenye Mwaka
Shahidi (Tigo): Mwaka inatofautiana na Barua ya Polisi waliyoleta
Kibatala: Ni sahihi kwamba Jalada ulilonukuu wewe ni tofauti ambalo hata polisi wamekuletea
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Ulitoa ufafanuzi wakati unaongozwa na wakili wa serikali kwamba umeulizwa barua kwa Jalada A wewe ukajibu Jalada B
Shahidi (Tigo): Hapana Sikusema
Kibatala: Twende eneo lingine, umetoa kielelezo namba P6 ni KYC. Nimesikia mnaulizana rekodi za NIDA Vs @Tigo_TZ Kwa kuwa Taarifa za Freeman Mbowe zipo NIDA, ni sahihi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: kwa hiyo kimsingi NIDA ndiyo Primary Source za Freeman Mbowe
Shahidi: Haupo sahihi
Kibatala: Basi niambie Uhusiano wa Tigo na NIDA katika KYC
Shahidi (Tigo): Kwa sababu sisi tuna chukua Data Kwao kimtandao
Kibatala: Kwa hiyo utakubaliana na Mimi NIDA ni Primary Source
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Usajili wa Tigo unaweza kutambulika bila Mtu Kusajiliwa NIDA
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: katika Ushahidi wako umezungumzia Lolote Kuhusu wewe Kusomea Mambo ya Data za NIDA
Shahidi (Tigo): Hapana Sikuzungumzia
Kibatala: Wewe unaweza Kuzungumzia suala la Server ya NIDA Kama siyo Administrator wa NIDA
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Kuna aina Ngapi za Server
Shahidi (Tigo): Email Based, Data Based Server
Kibatala: Nikisema LINU server unaelewa
Shahidi (Tigo): Ndiyo naifahamu
Kibatala: Ni nini
Shahidi (Tigo): Maelezo yake sifahamu
Kibatala: Ni Lenox au Linux
Shahidi (Tigo): Linux
Kibatala: huku Taja Window Server
Shahidi (Tigo): Sikusema
Kibatala: SQL Server Foft ware
Shahidi (Tigo): Fost ware
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Server ni Software au Hardware
Shahidi (Tigo): Hard Ware
Kibatala: Kuna Version kadhaa za SQL Software
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala tutajie The Latest SQL version
Shahidi (Tigo): Siwezi Kujua Kwa kweli
Kibatala: Sasa aliyemtajia Jaji Mambo ya SQL fotware ulilenga nini
Shahidi (Tigo): Kumuonyesha Jaji ni wapi nilipata Hizo Nyaraka
Kibatala: Wewe Hukutaka kabisa Jaji ajue Uimara, Uadilifu na Uimara wa hizo Software
Shahidi (Tigo): Sikumwambia
Kibatala: Je unajua The SQL Software 2019 ndiyo The best wewe utakataa?
Shahidi: SIWEZI KUJUA NDIYO MAANA NIMESEMA SIWEZI KUELEZEA HIYO
Kibatala: kwa Maelezo yako SQL Server Mnayotumia ni ya 2015
Shahidi: Nilisema ile ndiyo nilisoma Kozi ya introduction, tume update juzi
Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Umeupdate Juzi
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: VAPT ni nini
Shahidi: NI Watu wakujaribu Umadhubuti wa mifumo
Kibatala: Kutokana na Umuhimu huo ndiyo Maana Mkawafuata Ernest & Young Taasisi Kubwa, Mmechukua Kwa ajili ya Ulinzi wa Mifumo?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Sasa ulimwambia Mheshimiwa Jaji..?
Shahidi (Tigo): Siku Mwambia Exactly
Kibatala: Hatuna Kumwambia Exactly Wanasheria
Kibatala: Unafahamu DB2 software
Shahidi (Tigo): Siifahamu
Kibatala: Kwa hiyo wewe nikikwambia DB2 ndiyo madhubuti duniani kwa uwezo wake, huwezi kujua?
Shahidi (Tigo): Siwezi Kujua Kwa kweli
Kibatala: Na Unajua Kuwa SQL ni Moja software ya Bei Rahisi Duniani
Shahidi (Tigo): Inayoweza Kununulika (affordable)
Kibatala: Unafahamu Kwamba Tigo ni Reportimg Institution
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Martin Maranja Masese @IAMartin_ · 48m Kibatala: Mlishawahi Ku’ report Mambo yasiyofahaa Kuhusu Hiyo namba za simu
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Unafahamu Kuwa PEGASUS ni SoftWare Hatari sana Duniani Kwa ajili ya Kuingilia Mawasiliano wa mtu
Shahidi (Tigo): Hilo sifahamu
Kibatala: Makao Makuu ya Tigo yapo Karibu kabisa na Eneo la Usalama wa Taifa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Unafahamu Kuna Pesa Za Mteja Zimeibwa Kwenye huduma ya Kibubu ya tigo, Na Mwanasheria Pacience Mlowe ameleta Demand Notes kwenu
Shahidi (Tigo): Hapana Sifahamu
Kibatala: Nakupeleka Kwenye Detail ya Miamala ya pesa
Kibatala: Kuna Originating Number na Terminating Namba
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Wewe Ulionyeshwa hapa Mahakamani Kwamba hii Ndiyo Terminating Namba.?
Shahidi (Tigo): Sikuonyeshwa
Kibatala: unafahamu kuwa kuna Huduma ya Kurudisha Miamala
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa hiyo hatuwezi Kusema Details za kuanzia Tarehe 01.8.2020 kama tunazo hapa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa hiyo hatujui Kama Pesa hiyo huenda mbele Ilirudishwa, Si Ndiyo
Shahidi:Ndiyo Hatujui
Kibatala kamaliza kuuliza maswali ya Dodoso.. Anasimama sasa Wakili wa Serikali Kwa ajili ya Re examination..
WS : Nitakuuliza Kwa ufafanuzi na Pole Kwa Maswali..