
SHIRIKA lisilo ka kiserikali la Young and Alive initiative, linaloshughulika kutoa elimu jinsi kupambana na afya ya uzazi kwa vijana na jinsia, mapema jana Novemba 6, 2021 lilifanya mkutano na waandishi katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shell, ulipo Makumbusho, jijini Dar, kuhusiana na kutoa elimu ya uzazi na jinsia kwa vijana kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea ,ili vijana wapate elimu hiyo ambayo mara nyingi inakuwa ni ngumu kwa wazazi kuzungumza na watoto wao kutokana na mila na desturi zilivyo.
Hata hivyo shirika hilo pia limesistiza litafanya jitihada za kutoa elimu hiyo kupitia vyombo mbalimbali za habari ili kila kijana aweze kuelimika na hata kuwasiliana na vijana wanapopata changamoti mbalimbali,ili mwisho wa siku kuwe na kizazi chenye uzazi salama na kuepuka changamoto mbalimbali wanazokutana nazo vijana wakati wa uzazi.
Na Imelda Mtema