
KIJANA ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, anaye kadiliwa kuwa na umri wa miaka (25-30), amekutwa ameuawa na kutobolewa macho, katika ghuba la kuhifadhia uchafu lililopo maeneo ya Ngokolo mitumbani Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwinamila katika eneo hilo la tukio Amir Athumani, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.

Amesema baada ya kufika eneo la tukio majira ya saa moja asubuhi, ameukuta mwili wa kijana huyo akiwa ameuawa kinyama na kutobolewa macho, na watu ambao bado hawajafahamika.
“Tukio hili nila pili la watu kuuawa kwenye ghuba hili la uchafu, akiwamo na mtoto mdogo kuuawa na kuweka ndani ya boksi, hivyo naomba wananchi kama wana migogoro, watafute ufumbuzi na kuacha kujichukulia sheria mkononi,” amesema Athumani.