
MOTO mkubwa umeteketeza upande mmoja wa Soko la Gikomba jijini Nairobi na kuharibu mali ya thamani isiojulikana mapema leo Jumatatu, Novemba 8, 2021.
Saa 48 kabla, wafanyabishara walipata pigo baada ya Mamlaka ya jiji la Nairobi kupatiwa ruhusa na mahakama kuwaondoa baadhi ya wauzaji mitumba ili kutoa nafasi ya upanuzi wa kituo cha afya cha Pumwani Majengo Health Center.
Eneo la soko lililoungua lilikuwa lile la mitumba ambapo wafanyabiashara wengi huhifadhi mali yao. Wafanyabiashara waliowasili walikuwa tayari wamechelewa kuokoa mali yao huku ikiwa ni mabati yaliochomeka pekee ndio yaliosalia.
Gari la huduma ya Zima moto la jiji la Nairobi liliwasili katika eneo la tukio lakini moto huo tayari ulikuwa umesambaa kutokana na vibanda vya mbao vilivyotengenezwa.