×

TIRA, BOT Wavutiwa na Huduma Mpya ya Bima Benki ya Exim

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jafari Matundu alisema katika kufanikisha huduma hiyo benki hiyo tayari imekwisha waandaa vema baadhi ya wafanyakazi wake mahususi kwa ajili ya kutoa huduma kwa kushirikiana na kampuni za Bima 10 ambazo zinashirikiana na benki hiyo kuendesha huduma hiyo.

Dar es Salaam; Novemba 08, 2021: Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimeunga mkono ushirikiano unaoshuhudiwa hivi sasa baina ya taasisi za kifedha pamoja na makampuni ya bima nchini katika kutoa huduma mbalimbali za kibima huku zikionesha kuvutiwa  na huduma mpya ya bima ijulikanayo kama “Bima Tu, Malipo Tuachie” inayotolewa kupitia benki ya Exim Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha huduma za Bima kwa mabenki wa benki hiyo, Bw Melchizedeck Muro akizungumza kwenye hafla hiyo.

Wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo ya “Bima Tu, Malipo Tuachie”, iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa TIRA Bw Hillard Maskini pamoja nae Meneja wa Usimamizi wa Taasisi za Fedha wa BoT Bw Nassor Omary walisema ushirikiano huo pamoja na mambo mengine utaongeza wigo wa kuwafikia wateja na wanachi kwa ujumla na hivyo kukuza sekta ya bima  sambamba na kuboresha huduma za kibenki nchini.

Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa TIRA Bw Hillard Maskini akizungumza kwenye hafla hiyo

Katika kutekeleza huduma hiyo mpya  benki ya Exim imeshirikiana na kampuni 10 kubwa za bima nchini ili kuwaletea wateja wake huduma bora za Bima zikiwemo, Bima ya Afya, Bima ya safari na Bima ya Maisha ambazo zote zitatolewa pamoja chini ya benki hiyo.

Meneja wa Usimamizi wa Taasisi za Fedha wa BoT Bw Nassor Omary akizungumza kwenye hafla hiyo.

“Ushirikiano huu unaoendelea hivi sasa ni hatua nzuri zaidi kufikiwa katika historia ya utoaji wa huduma za kibima nchini. Ndio maana sisi kama wadau na wasimamizi wakubwa wa sekta hii ya Bima tunazipongeza sana taasisi za kifedha ikiwemo benki ya Exim kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kuwa kupitia ushirikiano kama huu utasaidia kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibima nchini,’’ alisema Bw Maskini aliemuwakilisha Kamishna wa TIRA Dkt. Mussa Juma.

Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda akizungumza kwenye hafla hiyo.

Alisema nia ya serikali kwa sasa ni kuongeza wigo wa mtandao wa utoaji huduma za bima kwa jamii ya watanzania ambao kwa sasa ni asilimia 28.6 tu ndio waliofikiwa na huduma hiyo.

“Hivyo basi nadiliki kusema kwamba  “Bima Tu, Malipo Tuachie” ni huduma inayoshabihiana na azma ya serikali ya kupanua ushiriki wa wananchi wengi zaidi katika huduma za bima. Zaidi naamini kupitia huduma hii tutafanikiwa kuvutia watanzania wengi kujiunga na huduma za bima kwa kuwa sasa hawatahofia suala malipo ya mkupuo kwa kuwa Exim mpo kazini leo kwa ajili ya kesho yao.’’ Alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni ya Bima nchini (ATI), Bw Khamis Selemani akizungumza kwenye hafla hiyo.

Kwa upande wake Bw Nassor pamoja na kupongeza ushirikiano huo, alisema BOT imekuwa ikiunga mkono huduma za Bima kupitia mabenki yaani Bancassurance kwa kuwa pia inaongeza tija kwa taasisi hizo katika kuwahudumia wananchi.

“Ongezeko la watumiaji wa huduma za Bima nchini kupitia katika taasisi za kifedha, pamoja na faida nyingine za moja kwa moja kwa wananchi wenyewe pia ni faida kwa wadau yaani mabenki, mashirika ya bima na serikali. Na hiyo ndio sababu BOT tumekuwa tukivutiwa na ushirikiano wa aina hii.  Hiki tunachokishuhudia leo kinatupa faraja na matumaini makubwa sana…hongereni sana,’’ alisema Bw Nassor aliemuwakilisha Naibu Gavana wa BoT Dkt. Bernard Kibesse.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa makampuni ya Bima yanayoshiriki katika kufanikisha huduma hiyo, wateja pamoja wafanyakazi wa benki hiyo.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jafari Matundu alisema katika kufanikisha huduma hiyo benki hiyo tayari imekwisha waandaa vema baadhi ya wafanyakazi wake mahususi kwa ajili ya kutoa huduma kwa kushirikiana na kampuni za Bima 10 ambazo zinashirikiana na benki hiyo kuendesha huduma hiyo.

“Si tu kwamba wafanyakazi wetu wamepatiwa mafunzo mahususi kufanikisha mpango huu bali pia wameidhinishwa na mamlaka husika kuwa wameiva katika kuwasaidia wateja wetu hususani katika utoaji wa elimu kuhusu huduma za bima wanazohitaji…kwa hiyo tumejipanga haswa,’’ alisisitiza.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa makampuni ya Bima yanayoshiriki katika kufanikisha huduma hiyo, wateja pamoja wafanyakazi wa benki hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo Mkuu wa Kitengo cha huduma za Bima kwa mabenki wa benki hiyo, Bw Melchizedeck Muro, alisema kupitia huduma hiyo benki ya Exim itatoa mikopo itakayowawezesha malipo ya huduma za bima za aina mbalimbali kupitia Kampuni 10 za bima zinazoshirikiana na benki hiyo na wakopaji wataendelea kulipa taratibu mkopo huku wakiendelea kunufaika na bima hizo.

Katika kutekeleza huduma hiyo mpya  benki ya Exim imeshirikiana na kampuni 10 kubwa za bima nchini ili kuwaletea wateja wake huduma bora za Bima zikiwemo, Bima ya Afya, Bima ya safari na Bima ya Maisha ambazo zote zitatolewa pamoja chini ya benki hiyo.

“Hiyo ndio sababu tukaamua kusema “Bima Tu, Malipo Tuachie”. Alisema Bw Muro huku akiyataja makampuni ambayo yanashirikiana na Exim kutoa huduma hiyo kuwa ni Jubilee Insurance, Fist Assurance, Heritage Insurance, GA Insurance, Alliance Life Assurance na Britam Insurance.

Mengine ni UAP Insurance, ICEA Lion General Insurance, Strategies Insurance, na Alliance Insurance corporation.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jafari Matundu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa TIRA, BOT na ATI wakati wa hafla hiyo. Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa TIRA Bw Hillard Maskini (wa pili kushoto), Meneja wa Usimamizi wa Taasisi za Fedha wa BoT Bw Nassor Omary (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni ya Bima nchini (ATI) Bw Khamis Selemani (Kushoto) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu (Kulia)

 Zaidi Bw Muro alibainisha kuwa katika utoaji wa huduma hiyo Benki hiyo imejipanga kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu huduma za bima ili kuondoa changamoto zinazotokana na ukosefu wa elimu hiyo miongoni mwa wateja wao.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa makampuni ya Bima yanayoshiriki katika kufanikisha huduma hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni ya Bima nchini (ATI), Bw Khamis Selemani wateja pamoja wafanyakazi wa benki hiyo.

Leave a Comment