×

50 Cent Aaishi na Risasi Kwenye Ulimi kwa Miaka 21

UNAAMBIWA ilikuwa ndinga moja kali inakatiza mitaa ya karibu kabisa na nyumba ya bibi yake mida fulani hivi, bila kuelewa hili wala lile, mshikaji alikuwa nje, zikasikika njugu zikimiminika, zilimpata kama risasi 9 na kumjeruhi sehemu mbali mbali ya mwili wake, na hapa alikuwa na umri wa miaka 25 tu.
Anasema ni moja ya matukio ambayo hawezi kusahau kabisa mpaka anakwenda kaburini, kwa sababu kwa vyovyote vile ingeondoa uhai wake, lakini bahati nzuri Mungu alikuwa upande wake, hivyo alisalimika, risasi zikapenya kwenye mikono, miguu, kifua mpaka kwenye shavu lake la kushoto na kumsababishia matatizo makubwa.
Si mwingine, huyu ni rapa Curtis James Jackson III maarufu kama ’50 Cent’ ambaye amesema kuwa bado mpaka hii leo anaishi na kipande cha risasi ndani ya ulimi wake ambacho kimeathiri kuongea kwake.
Rapa huyo amesema Daktari alihofia kutoa risasi hiyo kwa sababu ingeharibu ladha na kuleta madhara makubwa zaidi (kwahiyo huu ni mwaka wa 21 jamaa anaishi na kipande cha risasi kwenye ulimi). Vile ambavyo jamaa anaimba na kuongea ni sababu ya kipande cha risasi, lakini pia 50 Cent alisema kuwa hiyo ndio sauti inayofanya kazi, ile ambayo Mungu aliacha aifanye mpaka sasa.
50 Cent alilelewa katika kituo cha watoto yatima akiwa na miaka 8 baada ya mama yake mzazi kufariki ambaye alikuwa akijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya, 50 aliingia mtaani na yeye kuendeleza kile alichokuwa akifanya Bi mkubwa akiwa na miaka 12.
50 amekulia mtaani tu akiwa na ndoto siku moja atafanikisha na kufika kule ambako anahitaji kufika, kupitia kitabu cha “The 50th Law of Power” ambacho kimeandikwa kwa usaidizi wa Robert Greene imeandikwa kuwa 50 alikuwa mchakalikaji ambaye hakuhitaji kabisa maisha yake yote kuishia mtaani kama muuzaji wa dawa za kulevya kwahiyo alibadilisha upepo wa utafutaji wake wa mkwanja.
Muziki ulikuja baadae mengi kupitia nyimbo zake kuna line zinaongelea lifestyle yake na kupitia wimbo wa Ghetto Quran umeeleza kuhusu Kenneth McGriff ambaye ndiyo alihusika kumlipa kijana Darry akamtwange Risasi. Leo hii ni Muigizaji, mfanya biashara, Mwanamuziki na Producer pia.

Leave a Comment