JESHI la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu akiwemo Baba mzazi Kulwa Juakali (40) Mkazi wa Kijiji cha Lufubu wilaya ya Uvinza kwa tuhuma za kumpiga fimbo mtoto wake Mbaru Juakali ( 17) hadi kusababisha kifo chake huku chanzo cha tukio hilo nikumpiga mtoto huyo kumlazimisha kuolewa kwa mahari ya Ng’ombe 13 bila ridhaa yake.
“Binti alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake akilazimishwa kuolewa ambapo kulikua na ahadi ya kulipwa mahari ya Ng’ombe 13, na waliokua wakishinikiza aolewe ni wazazi na hao ndio walikua na uroho wa kupokea mahari ya hao Ng’ombe 13.
“Taarifa zilizopo binti huyu alikua anachumbiwa na wanaume watatu kwahiyo yule ambae game lilikua kubwa kwa Ng’ombe 13 huyo ndio alikua analazimishwa aolewe nae wakati binti hakuridhia na kupelelea kipigo,” James Manyama RPC Kigoma.
Polisi Kigoma wanasema upelelezi wa shauri hilo unaendelea watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria akiwemo Baba mzazi Kulwa Juakali (40), Baba mkubwa wa marehemu Shija Juakali (44) na Baba mdogo wa marehemu aitwaye Majiba Juakali ( 29) wote wakazi wa kijiji cha Lufubu wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
