×

Trugger_Tz Kufuata Nyayo za Harmonize

 
WASWAHILI husema “huwezi kuukimbiza upepo.” Pengine sifa yake kubwa ni kwamba hauonekani, ndiyo maana msanii TRUGGER_TZ ameamua kukimbizana na nyayo za msanii Harmonize katika kuyafikia mafanikio yake ya kimuziki.
 
TRUGGER_TZ ambaye baadhi ya wakazi wa Chamazi nje ya Jiji la Dar yaliko makazi yake humuita Nungunungu ameonesha nia hiyo alipofanya mazungumzo na Global muda mfupi baada ya kuachia ngoma yake aliyoipa jina la Hands Up Stand Up.
 
“Pamoja na kwamba ngoma hiyo iko kwenye mtindo wa TRAP na HIP HOP, lakini imepokelewa vizuri, malengo yangu kimuziki ni kufika mbali, nikimuangalia Harmo napata nguvu ya kusonga mbele kwa sababu naye kahaso kimaisha na kimuziki kama mimi.
 
Aliongeza kuomba sapoti ya mashabiki na kwamba wanaotaka kuwasiliana naye wampigie kwa amba za simu 0787939200 au kutembelea mitandao yake ya kijamii ya YouTube, Instagram na Facebook ambako anapatikana kwa jina la @trugger_tz

Leave a Comment