×

Dayna Nyange Aanika ‘Ugonjwa’ Wake Kwa Mwanaume

MAMBO vipi msomaji wa safu yako pendwa ya My Style, kama ilivyo kawaida huwa tunakutana hapa na kupiga stori mbili tatu na mastaa wa Bongo, ili kujua life style yao mbali na kazi wanazofanya ipoje.

 

Leo tupo na mwanamama mrembo kunako gemu ya muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’ ambaye amefunguka mambo mengi usiyoyajua kutoka kwake, nini anapenda na nini hapendi, ungana nami hapa chini kwa mahojiano kamili:

My Style: Unajisikiaje kuwa mama?

Dayna: Ni raha sana siwezi hata kuelezea, naweza kusema namshukuru Mungu kwa hii baraka ambayo nimeipata

My Style: Wewe ni mama wa watoto wangapi?Dayna: Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kike anaitwa Rahma?

My Style: Jambo gani baya ambalo umewahi kupitia kama mtoto wa kike na hautamani na binti yako aje alipitie?

Dayna: Mimi ni mtu ambaye huwa nakuwa muoga sana kufanya maamuzi, sina kitu kingine zaidi ya hicho kwa sababu hayo mambo mengine ni changamoto tu za kawaida, hivyo natamani mwanangu aje kuwa na maisha mengine mbali na haya ya mitandaoni kwa sababu yatamfanya kuwa huru.

My Style: Umeshawahi kumkosea mtu kwa kumjibu vibaya, halafu mwisho wa siku ukajutia kwa ulichokifanya?

Dayna: Inawezekana kwa sababu hakuna mkamilifu hapa duniani, lakini mara nyingi mimi ni mtu wa kukaa peke yangu na huwa nachagua sana mtu wa kuongea naye, kiufupi sina marafiki nadhani hilo ndio linalonisaidia, labda kwenye uhusiano ndio huwa kuna muda nafanya maamuzi tofauti halafu baadaye naanza kujuta.

 

My Style: Kitu gani ambacho hakikosekani kwenye dressing table yako?

Dayna: Perfume na vitu vingine vyote vinavyohusu urembo havikosekani kwenye dressing table yangu.

 

My Style: Unaweza kutuambia gharama ya hayo meno ya dhahabu uliyovaa?Dayna: Ni dola 300, sawa na Shilingi 700,000.

 

My Style: Kwa nini uliamua kuyaweka?Dayna:Niliwahi kumuona Drake ameweka hiki kitu nikapenda sana, na tangu nimeweka ni miaka kadhaa imepita yaani ni permanent kabisa ila nikitaka kutoa nina uwezo wa kutoa.

My Style: Ok, uliweka ukiwa wapi?Dayna: Niliweka nikiwa Afrika Kusini wakati nafanya video ya Chovya.

My Style: Wewe ni chizi nini?

Dayna: Aisee mimi ni chizi nywele (Wigi) halafu iwe ndefu yaani hapo huniambii kitu.

 

My Style: Nywele yako ya bei mbaya ulinunua shilingi ngapi?Dayna: Nimeshaw ahi kununua nywele ya inch 35 kwa shilingi Milioni 2.8.

 

My Style: Mtandao gani wa kijamii ambao huwezi ukapitisha siku bila kuingia?Dayna: WhatsApp, kwa sababu nawasiliana na watu wengi, tofauti na mitandao mingine.

 

My Style: Unapenda kufanya kazi gani unapokuwa umetulia nyumbani na familia yako?

Dayna: Nikiwa nyumbani napenda kupika na kufua.

 

My Style: Unakunywa pombe?

Dayna: Hapana, ila wine naonja kidogo.

My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

 

Dayna: Starehe yangu kubwa ni kula, tena vyakula vizuri.

My Style: Ukipewa nafasi ya kurudisha kitu ambacho umewahi kukipoteza huko nyuma utarudisha kitu gani?

 

Dayna: Natamani ningemrudisha shangazi yangu kwa sababu yeye ndio alinilea tangu nikiwa mdogo, lakini ghafla akafariki dunia, niliumia sana.

 

My Style: Unapenda ku-date na mwanaume mwenye vigezo vipi?

Dayna: Napenda mwanaume anayejielewa na awe smart.

 

My Style: Jambo gani huwa linakukera sana pindi unapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Dayna: Huwa sipendi uongo kwa sababu binafsi nikiwa na mtu huwa sipepesi macho kuangalia sehemu nyingine.

 

My Style: Kati ya rafiki mchawi au mbea utachagua yupi?

Dayna: (Anacheka) bora mchawi kwa kweli nitasali nitapambana naye, lakini sio mbea hawa watu ni wabaya sana.

 

My Style:Mwanaume mwenye show off (anayependa kujionyesha) au muhuni?

Dayna: Mwenye show off huyu tutavumiliana, ila muhuni hapana kuna magonjwa siku hizi.

 

My Style: Umeshawahi kwenda kwa mganga ili kuweka mambo yako sawa?

Dayna: Hapana, sijawahi kwenda hata mara moja

 

My Style:Umeshawahi kumtongoza mwanaume?Dayna: Hapana sijawahi.

My Style: Ikitokea umempenda mwanaume kimapenzi huwa unafanyaje ili ajue umempenda?

 

Dayna: Ikitokea nimempenda nitatengeneza mazingira ya kumfanya avutiwe na mimi, ili mwisho wa siku yeye ndio anianze.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Leave a Comment