×

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda cha Vifaa vya Kisasa vya Ujenzi

Waziri Mkuu Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda hicho.

 

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo amezindua Kampuni ya Kutengeneza Vifaa vya kisasa vya Ujenzi pamoja na kujishughulisha na ujenzi iitwacho Sika kutoka nchini Switzerland ambapo hapa nchini ipo Salasala, Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akipata maelekezo ya bidhaa zinazozalishwa kwenye kampuni hiyo.

 

 

Waziri Mkuu Majaliwa baada ya kufika kwenye kiwanda hicho alitembezwa maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho na kujionea jinsi wanavyotengeneza vifaa vyao kwa teknolojia ya kisasa.

Hapa akioneshwa mchanga maalum ulioandaliwa kwaajili ya kusakafia ukutani na sakafuni. kUshoto Mbunge wa Kawe naye akisikiliza kiumakini maelekezo yanavyotolewa.

 

 

Baada ya kukagua sehemu mbalimbali za uzalishaji wa vifaa hivyo na kuridhishwa na mazingira yake aliusifu uongozi wa kampuni hiyo na kuwashauri wananchi kuiunga mkono kampuni hiyo ikiyowekeza hapa nchini.

Maofisa wa kampuni ya Sika wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya Waziri Mkuu kuzindua kampuni hiyo.

 

 

Akizungumza kwenye risala yake Waziri Mkuu Majaliwa amesema kitendo cha Kampuni ya Sika kuja kuwekeza hapa nchini tayari ni faida kwa wananchi mmojammoja kujipatia kipato kwa njia ya ajira na serikali ya kujipatia kipato kupitia kodi.

Waziri Mkuu Majaliwa akimpa cheti mmoja kati ya waliotangazwa wafanyakazi bora.

 

 

“Kama siku zote Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza sera ya kuwavutia wawekezaji wa viwanda hata hivyo tunawaona Sika ni kama mnaiunga mkono serikali yetu kwa kuja kuwekeza hapa nchini.

Waziri Mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Sika na viongozi wa serikali na wengineo.

 

Akiisifu Kampuni hiyo, Waziri Majaliwa ameipongeza kwa kitendo chake cha kuajiri Watanzania kwa asilimia kubwa na kuwaomba kuangalia na suala ya kuwaajili walemavu katika shunghuli wanazozimudu.

 

Hata hivyo Waziri Majaliwa ameiomba kampuni hiyo kuangalia na uwezekano wa kuwaajiri walemavu katika nafasi wanazozimudu.

 

Hatika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josepaht Gwajima, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe na wengineo.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL  

Leave a Comment