×

Coletha: Mume wangu Mzungu

MWIGIZAJI wa kitambo wa Bongo Movies tangu enzi za Kaole, Coletha Raymond amemwaga sifa kama zote kwa mumewe kwamba ni mtu mzungu f’lani ambaye ni wa kipekee aliyemuona chini ya jua na aliyemuonesha mapenzi ya kweli.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Coletha anasema kuwa, anamshukuru mno Mwenyezi Mungu kumpata mume mwenye mapenzi ya kweli na kujua thamani yake kama mwanamke.

“Yaani huku duniani wanawake wengi wanapata taabu sana kupata wanaume wa kweli na wenye mapenzi ya dhati, ila mimi namshukuru sana Mungu kwa kunipa mume bora maishani na mwenye kuthamini kazi yangu,” anasema Coletha ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment