
KAMPUNI ya Peak Time Promotion kupitia kwa mkurugenzi wake, Kapteni Selemani Semunyu imeweka wazi kuwa pambano la usiku wa mabingwa litaangaliwa kwa kiingilio cha Sh 10,000 pekee kwa lengo la kutoa nafasi kwa wadau kusherehekea mafanikio ya mchezo huo kwa mwaka 2020.
Katika hilo litawakutanisha mabondia wa Tanzania ambao ni Twaha Kiduku, Mfaume Mfaume, Seleman Kidunda, Dullah Mbabe, Tonny Rashidi, Ismail Galiatano, Issa Nampepeche, Haidari Mchanjo, Lorent Japhet na Juma Choki.

Pambano hilo litafanyika Desemba 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Next Door Masaki chini ya udhamini wa ya udhamini wa Gazeti la Spoti Xtra, +255 Global Radio, Euromax, Kebbys Hotel, Presicion Air, Azam TV, Clouds Media, na Uhuru FM.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kapteni Semunyu alisema kuwa lengo la kuweka bei ya kawaida katika pambano hilo ni kuweza kufanya mashabiki wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi katika kusherehekea mafanikio ya mchezo huo kwa mwaka huu.

“Maandalizi yanakwenda vizuri lakini safari katika suala tiketi tumeanza mapama kwa sababu zinapatika kwa bei ambayo kila Mtanzania zitamfanya aweze kufika Next Door kuangalia muendelezo wa mapinduzi wa ngumi za kulipwa ndani ya Usiku wa Mabingwa lakini kusherekea kwa pamoja mafanikio ya mchezo wenyewe.
“Tiketi zinapatika kwa bei ya Sh 10,000 kwa mzunguko, lakini kwa watakaweza kununua mapema, Sh 50,000 kwa Kawaida na Sh 100,000. Mauzo yameanza kufanyika katika vituo Vunja Bei na Vunja Bei Toto (Sinza), Shishi Food (Kinondoni), Dicksound (Magomeni),Kaites Lounge Tabata na Cake City (Njia Panda ya Salasala) AU wanaweza kutupigia simu kupitia namba 0655712777,” alisema Kapteni Semunyu.

Katika pambano hilo Mfaume Mfaume atapanda ulingoni kuzichapa na Chikondi Makawa kutoka Malawi wakatiTwaha Kiduku atazichapa na Guy Tshimanga Tshitundu wa DR Congo lakini Abdalah Pazi ‘Dullah Mbabe’ atamaliza utata na Simon Tchetcha wa Malawi.
Tonny Rashid atatetea mkanda wake wa Abu dhidi ya Hassan Milanzi wa Zimbambwe wakati Seleman Kidunda kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) atazichapa na Limbani Masamba wa Malawi.
Wengine ni Ismail Galiatano kutoka JWTZ atazitwanga na Israel Kamwamba wa Malawi huku Haidary Mchanjo na Loren Japhet.