The House of Favourite Newspapers

Kiiza: Simba imebadilika, inakuja kivingine

0

HAMISI-KIIZAStraika Hamis Kiiza.

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
BAADA ya kufanikiwa kuwasajili Brian Majwega, Paul Kiongera na Danny Lyanga, straika Hamis Kiiza wa Simba amesema kikosi chao kimebadilika na sasa kina mwonekano mpya wa ushindi.
Majwega ni kiungo mshambuliaji kama ilivyo kwa Kiongera wakati Lyanga ni straika, wengine waliosajiliwa na Simba wakati huu ni beki Novatus Lufunga wa African Sports na straika Hija Ugando. Kiiza raia wa Uganda aliyewahi kuichezea Yanga, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, ujio wa wachezaji hao utaiongezea nguvu Simba na anaamini pia utamuongezea kasi ya ufungaji.
Hadi sasa Kiiza amefunga mabao nane sawa na Donald Ngoma wa Yanga wakati straika wa Stand United, Elias Maguri akiongoza kwa kufunga mabao tisa katika mechi 11.
Alisema Simba sasa inakuja kivingine kwani usajili uliofanywa umezingatia mahitaji ya timu na mashabiki wategemee mambo mazuri kutoka kwao.

Leave A Reply