
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa baada ya kutoa sare katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo hawatahitaji matokeo kama hayo katika mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya Kwanza zaidi ya ushindi tu.
Yanga katika mchezo uliopita walitoa sare dhidi ya Namungo kwa bao 1-1, Novemba 30 wanatarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza mkoani Mbeya.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa: “Mchezo uliopita tulitoka sare na Namungo, mchezo unaofuata tutacheza na Mbeya Kwanza tukiwa ugenini, hatuhitaji jambo lingine zaidi ya ushindi, Wanayanga wote pia hawahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi na ndio maana tunawaambia kuwa Mbeya Kwanza watatusamehe.
“Najua kila mchezo wa ligi kwa sasa ni mgumu, hivyo haitakuwa rahisi kupata ushindi lakini hilo halitatuzuia sisi kushindwa kupata ushindi, tumejiandaa vya kutosha kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ambayo ni ushindi,” alisema Bumbuli.
Stori na Marco Mzumbe, Dar es Salaam