×

Kanye West Alilia Ndoa na Kim Kardashian

 

RAPA maarufu duniani kutoka pande za Marekani Kanye West amekiri kuwa alifanya makosa katika ndoa yake na Kim Kardashian na kusema kuwa ni mpango wa Mungu yeye na mkewe Kim kurudiana na kutengeneza maisha kwenye nyumba pamoja na watoto wao.

 

Akiwa mjini Los Angeles kwenye sherehe za shukrani, Kanye West, 44 alisema anaamini kuwa atarudiana tena na mke wake Kim Kardashian licha ya mwanamitindo huyo na nyota wa kipindi cha ‘Keep up with the kardashians’ kuwa katika mahusiano na muigizaji Pete Davidson.

 

Kanye ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy aliongeza kuwa amefanya vitu vingi hadharani ambavyo havikubaliki akiwa kama mume wa mtu.

“Mungu anataka kuona tunafufua mahusiano yote haya, tunafanya makosa. Nimefanya makosa.  Lakini sasa kwa sababu yoyote ile sikujua nitakuwa mbele ya kipaza sauti hiki, lakini nipo sasa kubadilisha kauli zangu” alisema Kanye.

 

Akizungumza kuhusu mpenzi mpya wa Kim na nyota wa kipindi cha SNL, Kanye alisema hatoruhusu televisheni ya E kuandika simulizi juu ya familia yake, “sitaruhusu Hulu iandike simulizi ya familia yangu… mimi ni mchungaji katika nyumba yangu.”

 

Aliongeza Kanye Aliendelea kueleza kuwa ana imani na Mungu kuwa ataungana tena na mke wake na watoto nyumbani, na kuanza kusambaratisha matendo ya shetani.

 

“Kama kuna adui anaweza kutenganisha KIMYE, basi kutakuwa kuna mamia ya familia ambazo zinahisi kuwa kutengana ni sawa. Lakini wakati Mungu analeta KIMYE pamoja, kuna mamia ya familia ambazo zinashawishika kuona tumeweza kushinda utengano huu, vurugu za shetani ambazo zinatumia mtaji kuweka watu katika taabu,” anasema Kanye.

 

Leave a Comment