×

Wizkid Msanii Bora Apple Music

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid ametangazwa kuwa msanii bora wa mwaka barani Afrika ‘Apple Music Artist of the Year’, huku msanii The Weekend kutoka nchini Marekani akitangazwa kuwa Msanii Bora wa Mwaka Duniani kote.

 

Wizkid ni mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika, ambaye amefanya kazi na Drake, Skepta na Chris Brown. Mwanamuziki huyo wa Nigeria alipata mafanikio ya kikanda mnamo mwaka 2011 kupitia wimbo wake maarufu uitwao ‘Holla at Your Boy’, ambao unapatikana kwenye albamu yake ya kwanza iitwayo “Superstar.”

 

Wizkid alianza kuvuma na kuupenyeza muziki wake duniani kote kuanzia mwaka 2016 baada ya kushirikishwa na msanii Drake kwenye wimbo wake “One Dance,” ambao ulifanikiwa kupanda hadi nafasi za juu kwenye chati za Billboard katika nchi takribani 15 Duniani.

 

Mwaka huu 2021, Wizkid amekuwa msanii wa Kiafrika aliyesikilizwa zaidi barani Afrika kupitia Apple Music na kuorodheshwa kwenye chati 100 bora za kila siku katika nchi takribani 60, ikiwa ni pamoja na kuchezwa kwake kila mwezi kwenye Apple Music kukua kwa zaidi ya asilimia 250 nje ya mipaka ya Afrika.

 

Pia ameshirikishwa kwenye Apple Music’s Today’s Hits and R&B Now playlists, , na amekuwa mgeni wa mara kwa mara kwenye vipindi vya Apple Music Radio, vikiwemo “Africa Now Radio,” “The Ebro Show,” “New Music Daily with Zane Lowe,” na “Ovo Sound Radio.”

Leave a Comment