×

Rais Samia Awawakia TIC Kisa Mwekezaji Huyu – Video

RAIS Samia ametoa maagizo makali kwa bodi ya uwekezaji nchini TIC kujitathimini sambamba na kubadilisha mifumo ya uhakiki wa taarifa za wawekezaji ili kurahisha zoezi hilo kufanyika kwa haraka.

 

Ametoa agizo hilo wakati akizindua kiwanda cha kuzalisha nyaya za mkongo wa mawasiliano cha Radda Fiber kilichopo Mkuranga, mkoani Pwani mapema Desemba 03, 2021.

 

Rais Samia amekemea ucheleweshwaji unaofanywa na Bodi hiyo hasa kwa waekezaji wazawa kwa kile alichokiita kuwa ni dharau kwa kuona kuwa wazawa hawana uwezo wa kufanya uwekezaji mkubwa.

 

“Jina Ramadhani Hassan Mlanzi bilashaka pale TIC (Kituo cha Uwekezaji Tanzania) walimtizama mara tatu tatu. pengine walimuona ni tapeli, pengine walimuona ni dalali, pengine walimuona ni muongo kwa sababu ya jina tu na kwamba ni Mtanzania.

 

“Kumbe wange kwenda naye haraka haraka ufunguzi wa kiwanda hiki ungefanyika miaka minne mitano nyuma. Tungekuwa tungeanza uzalishaji na Tanzania inatajika kwa uzalishaji wa hiyo biashara Afrika na Duniani. Lakini kwa sababu ya jina, Ramadhani Hassan Mlanzi basi unaanza kuzarau tu.

 

“Ndugu zangu, Mh Waziri naomba muache hizo kasumba. Kunawatanzania wengi wameshatembea wameshaona na wamepata mitaji naomba muwakumbatie kwa majina yoyote yale. Ndugu yangu nikupe pole ya mabonde na milima lakini nikupongeze.

 

“Nawaomba TIC mbadilike, huyu muwekezaji ameanza kuhangaika na nyie tangu mwaka 2015 hadi hii leo tupo hapa 2021 ni miaka sita, mlitazama jina mkaona ni ‘Hassan Ramadhani Mlanzi’ mkadharau matokeo yake mmechelewesha uwekezaji mkubwa namna hii, hii haipendi hata kidgo, mnataka hadi muone majina ya Johson wazungu wazungu ndio mharakishe,” amesema Rais Samia.

 

Aidha amewataka kuacha michezo hiyo mara moja kwani wanacheewesha maendeleo ya taifa kwa fikra potofu.

“Naomba muache hizo kasumba, acheni kufanya kazi kwa kutazama majina, wapeni wazawa kipaumbele na muharakishe maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla,” amesisitiza Mkuu huyo wa Nchi.

 

Ameongeza kusema kua Serikali imejipanga kufanya kazi bega kwa bega na kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya Km elfu 24 za nyaya sawa na Kilomita elfu mbili kwa mwezi.

Leave a Comment